VIDEO: MH,FESTO SANGA AIBUA UFISADI WA ZAIDI YA BILLION 200 FEDHA ZA HALMASHAURI NCHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 15, 2022

VIDEO: MH,FESTO SANGA AIBUA UFISADI WA ZAIDI YA BILLION 200 FEDHA ZA HALMASHAURI NCHINI


Mbunge wa Makete Mh Festo Sanga akichangia bajeti ya Wizara ya TAMISEMI Bungeni jijini Dodoma Aprili 14,2022 ndipo akaibua ufisadi mkubwa wa fedha za Umma zinazotengwa kwa ajili ya Vijana,wanawake na Walemavu yaani asilimia 10


Mbunge wa Makete Mh Festo Sanga akiwasili viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Aprili 14,2022


Mbunge wa Makete Mh Festo Sanga

Na Mwandishi wetu ,Bunge Dodoma

Mbunge wa Makete Mh Festo Sanga akichangia bajeti ya Wizara ya TAMISEMI , ameibua ufisadi mkubwa wa fedha za Umma zinazotengwa kwa ajili ya Vijana,wanawake na Walemavu yaani asilimia 10.

Mh. Sanga anasema tangu Mwaka 2017/2018 Serikali kupitia Halmashauri nchini imekopesha zaidi ya Bilioni 300 kwa Makundi ya Vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu.

Katika fedha hizo Serikali imefanikiwa kurejesha kiasi cha Billion 96 tu, fedha zingine zote zimezama kwenye mifuko ya watu wahuni".

Mh Spika nimefuatilia kwa ukaribu, Vijana wengi hawapati mikopo hii, akina mama wengi hawapati wala walemavu, Fedha hizi zinachukuliwa na wanasiasa, watumishi wa Serikali wanaounda vikundi "fake" na kujichotea fedha, zaidi watu wenye Mtandao na Halmashauri wanatumia vijana wasiokuwa na uelewa wanawandikisha kwenye Vikundi na kujipatia fedha kinyume na utaratibu".

Naomba kutoa mfano kwa sasa " Mkoa wa Dar Es salaam, tangu mwaka 2018 wamekopesha 52 Bilioni na wamefanikiwa kurejesha Billion 14.8 zingine zimepigwa, Mkoa wa Mbeya wamekopesha 12.9 Bilioni wamerejesha Bilioni 7.5 tu, zingine zipo mikononi mwa watu

Mkoa wa Geita wamekopesha Bilioni 6 na wamerejesha Bilioni 3.6 tu.

Mkoa wa Pwani wamekopesha Bilioni 11.4 wamerejesha Bilioni 4.1 tu zingine zimepigwa.

 Mkoa wa Arusha wamekopesha Bilioni 12.7 na wamerejesha Bilioni 5 tu.

 Hii ni Mifano tu Mheshimiwa Spika, fedha hizi zimekwama mikononi mwa watu wabaya wenye kuhujumu uchumi wetu.

Fedha hizi zingetumika kuwasaidia Vijana kuanzisha miradi mbalimbali ikiwepo kuwanunulia Mashine za Kufyatua tofali, viwanda vidogo n.k lakini zimeingia kwa watu ambao sio wema.

Naomba serikali iunde timu, wasake fedha hizi mali ya Watanzania zikafanye kazi iliyokusudiwa".


No comments:

Post a Comment