![]() |
| Mtaalam wa Saikolojia kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) Richard Haule akitoa ushauri wa kisaikolojia kwa wanafunzi waliokuwa wakisoma nchini Ukraine. |
![]() |
| Baadhi Wanafunzi waliosoma Ukraine pamoja na wazazi wao waliofika katika mkutano na Wadau wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Dar Es salaam. |
Na ISW Dar Es Salaam
Wahadhiri wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, ISW ambao pia ni wataalam wa saikolojia wametoa huduma ya ushauri wa kisaikolojia kwa wanafunzi wa kitanzania waliokuwa wanasoma nchini Ukraine katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania.
Huduma hiyo imetolewa Aprili 09,2022 mkoani Dar Es Salaam katika mkutano maalum uliowakutanisha na uongozi wa Wizara ya Elimu, Mwenyekiti wa kamati ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi ,Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Global Education Link na wataalamu wa saikolojia kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii iliyo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum.
Akitoa elimu hiyo Mtaalam wa Saikolojia kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii Richard Haule aliwashauri wanafunzi hao wasifuatilie habari za vita ili wasahau hali na Madhira waliyopitia pindi wapo Ukraine.
Amewataka kujishughulisha kazi mbalimbali na kushiriki michezo,shughuli za kijamii ili kusahau masuala ya vita.
"Wazazi, huu sio muda wa kulaumiana na watoto bali ni muda wa kutulia kimawazo ili kutafuta namna bora ya kutumia fursa zinazokuja za kimasomo na maisha kwaajili ya watoto wenu, ili kuona njia bora ya kut ndoto zao ambazo lazima ziendelee bila ya kukatishwa tamaa na janga la vita. Wazazi msikate tamaa kuendelea kuwagharamia masomo watoto wenu" alisema Haule.
Kwa upande Mwanafunzi wa udaktari wa tiba za binadamu na upasuaji mwaka wa pili aliyekuwa akisoma Sumy state university nchini Ukraine Franco Macho ameshukuru sana elimu na ushauri wa kimawazo waliopata kutoka kwa wanasaikolojia na kusema imesaidia sana kwasababu hawakuwa sawa na elimu hii imewapa mwanga na matumaini mapya.
"Baada ya vita kuanza, nilikuwa katika hali ya kukataa kama kweli kuna vita na ninatakiwa kuondoka, nilimwambia baba yangu sirudi Tanzania vita itaisha tuu, kumbe sikuwa sawa mpaka Mama alipoongea na mimi sana na kukubali kurudi nyumbani." Alisema Franco Macho
Wakiongea katika mkutano huo wazazi wa wanafunzi hao ambao waliambatana nao katika mkutano huo wameelezea jinsi ambavyo watoto wao hawapo katika hali ya kawaida kutokana na athari ya vita, hali ya kukatishwa masomo ghafla wengi wao imewafadhaisha sana, na baadhi wamekata tamaa ya kuendelea kusoma kwa kutokujua hatima yao ya kimasomo, wapo ambao hawatoki ndani na hawana hamu ya kula walisema.





No comments:
Post a Comment