WATUMISHI WA UMMA SASA KUTATHMINIWA UTENDAJI KAZI KIELETRONIKI KUANZIA JULAI MOSI MWAKA HUU-MH.MHAGAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 9, 2022

WATUMISHI WA UMMA SASA KUTATHMINIWA UTENDAJI KAZI KIELETRONIKI KUANZIA JULAI MOSI MWAKA HUU-MH.MHAGAMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Joyce Ndalichako (Kulia) wakiwa katika Mkutano na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kuhusu mtazamo wa serikali ya Awamu ya sita katika Uimarishaji wa Utumishi wa Umma unaowajibika kwa hiari na Matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji na utoaji Huduma bora katika Utumishi wa Umma,tarehe 9 Aprili, 2022 Jijini Dodoma.


Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya (wa kwanza kulia ) akifuatilia Mkutano na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kuhusu mtazamo wa serikali ya Awamu ya sita katika Uimarishaji wa Utumishi wa Umma unaowajibika kwa hiari na Matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji na utoaji Huduma bora katika Utumishi wa Umma,tarehe 9 Aprili, 2022 Jijini Dodoma.


Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Rashid Mtima (Kushoto) akifuatilia Mkutano na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kuhusu mtazamo wa serikali ya Awamu ya sita katika Uimarishaji wa Utumishi wa Umma unaowajibika kwa hiari na Matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji na utoaji Huduma bora katika Utumishi wa Umma,tarehe 9 Aprili, 2022 Jijini Dodoma

Na Okuly Julius, Dodoma 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh.Jenista Mhagama amesema serikali inatarajia kuanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa (PEPMIS) kwa ajili ya kufanya tathimini ya hali ya watumishi wa umma kwa uwazi ili kuondokana na changamoto zilizokuwepo katika mfumo wa awali ifikapo Julai Mosi mwaka huu.

Ameyasema hayo hii leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuhusu mtazamo wa serikali ya awamu ya sita katika uimarishaji wa utumishi wa umma unaowajibika kwa hiyari na matumizi ya mfumo wa Tehama katika utendaji na utoaji huduma bora katika utumishi wa umma.

“Kuanza kutumika kwa mfumo huo ni utekelezaji wa agizo la Rais, Samia Suluhu Hassani alililolitoa kwa ofisi hiyo ili kuondoa changamoto za usimamizi wa utendaji kazi zilizojitokeza katika utekelezaji wa mfumo wa awali wa OPRAS, ambao haukuakisi hali halisi ya utendaji kazi wa watumishi hali iliyoleta hisia za kupendeleana au kuoneana na kutokutumika kwa matokeo ya utendajikazi katika kufanya maamuzi ya kiutumishi,Amesema Mhagama

Waziri Mhagama ameongeza kuwa serikali imekuwa ikifanya mabadiliko mengi yakiwemo ya kimfumo pamoja na ajira pia ni chachu ya maendeleo hata katika vyama vya wafanyakazi .

“Kwa mfano wiki ijayo Mheshimiwa Rais ametoa kibali cha kuajiri watumishi 32,000 ,hivi hapo na nyie vyama vya wafanyakazi mtakuwa mmeula kwa kuwa pia atakuwa amejenga nguvu ya kutosha kwa wafanyakazi kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi na mambo mengine kupitia wananchama yataongezeka na kuimarika .”amesema na kuongeza kuwa

“Ndio maana Ofisi yangu tumepokea maelekezo ya Rais ya kuihakikisha tunaweka mifumo imara itakayotuwezesha pia kufikia mipango mbalimbali ya maendeleo kutokana na utendaji mzuri kwa watumishi wa umma.”amesema

Amesema,Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma imeendelea kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandao na kujenga mifumo ya TEHAMA inayohusu uendeshaji wa Serikali wa kila siku na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa umma.

Mhagama amesema,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imefanikiwa kujenga Mfumo wa Sema na Waziri , Mfumo wa e-mrejsho, Mfumo wa Dawati la Huduma kwa Mteja maarufu kama UTUMISHI Call Centre ,Mfumo maalum wa Tathmini ya hali ya Mfumo wa Huduma Mtandao kwa Watumishi (Watumishi Portal).

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Joyce Ndalichako amebainisha kuwa pamoja na juhudi za serikali za kupima utendaji kazi serikalini Rais amelekeza ushirikishwaji wa Vyama vya Wafanyakazi ili waendelee kuwa daraja kati ya waajiri na Wafanyakazi kwa kuchochea na kuhimiza utamaduni kwa Wafanyakazi kudai haki na kutimiza wajibu wao.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu imeendelea kutekeleza maagizo ya Rais kwa kukamilisha Mfumo wa Kielektroniki wa utoaji wa Vibali vya Kazi kwa raia wa kigeni ambao umepunguza muda wa kushughulikia maombi ya vibali vya kazi kutoka siku za kazi 14 hadi siku 7.

Naye Rais wa shirikisho la wafanyakazi nchini TUCTA Tumaini Nyamhokya amesema,wao kama viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanachopenda ni wafanyakazi kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii na kwamba kinachotakiwa mifumo isiwe ni ya kunyanyasa wafanyakazi hasa kuwatumikisha zaidi ya muda wa kazi na bila mwajiri kutambua hilo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) Deus Seif amesema,mfumo wa awali wa OPRAS ulikuwa na changamoto nyingi hasa kwa walimu huku akisema anaamini mfumo unaokuja wa upimaji kazi utaweka mazingira sawa kwenye kupima utendaji kulingana na mazingira ya halisi na hivyo kufanya watumishi wa umma waufurahie utumishi wao.

No comments:

Post a Comment