Na Okuly Julius Dodoma
Dkt.Mpango ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifunga kilele cha wiki ya ubunifu kilichokwenda sambamba na mashindano ya kitaifa ya ubunifu ya sayansi ,teknolojia na ubunifu (MAKISATU) na utoaji wa tuzo kwa wabunifu waliofanikiwa kushinda katika mashindano hayo
Pia Dkt.Mpango ametoa rai kwa watanzania kutoa kipaumbele kwa kununua na kutumia mashine na bidhaa mbalimbali zinazotokana na wabunifu wa ndani maana kwa kufanya hivyo itasaidia kukuza mnyororo wa thamani na soko la ndani,kutengeneza fursa zaidi za ajira kwa watanzania na kuongeza kipato na kusaidia kupata vipuri vinavyohitajika kufanya ukarabati.
Pia ameongeza kuwa serikali inatambua umuhimu wa matumizi wa sayansi ,teknolijia na Ubunifu katika ujenzi wa uchumi imara na endelevu kama ilivyoainishwa kwenye dira ya taifa ya maendeleo ya 2020-2025 na ilani ya uchaguzi ya chama cha mpinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 ibara ya 102 inyoelekeza serekali kuhakikisha kuwa sayansi,teknolojia na ubunifu vinatumika kikamilifu katika kuendesha sekta ya kukuza uchumi.
Ameipongeza Wizara ya elimu kwa kuja na kaulimbiu yenye kuonesha taswira ya wiki hii ya ubunifu kuwa ni kwa ajili ya maendeleo endelevu na matunda ya bunifu hizi zitaanza kuonekana mapema tu kwa watanzania.
“Nimevutiwa sana na kaulimbiu ya mwaka huu inayosema UBUNIFU KWA MAENDELEO ENDELEVU inatukumbusha kuwa ubunifu na uvumbuzi wa teknolojia mbalimbali na matumizi yake ndio nyenzo ya uhakika ya kuharakisha maendeleo endelevu”amesema Dkt.Mpango
Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa lengo kubwa la Maonesho haya ya Ubunifu (MAKISATU) ni kufumbua akili za vijana wa kitanzania kuanza kuwaza kujiajiri kupitia bunifu mbalimbali na kuondokana na dhana ya kuwaza kuajiriwaa mara wanapohitimu vyuo mbalimbali hapa nchini.






No comments:
Post a Comment