HAKIKISHENI MNATENGA FEDHA KWA AJILI YA MASUALA YA LISHE-PROF.SHEMDOE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 25, 2022

HAKIKISHENI MNATENGA FEDHA KWA AJILI YA MASUALA YA LISHE-PROF.SHEMDOE



Okuly Julius Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Prof.Riziki Shemdoe amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatekeleza kutenga na kupekeka fedha Tsh.elfu moja kwa kila mtoto zinazohusiana na masuala ya lishe ili kupunguza utapiamlo nchini.

Prof.Shemdoe ametoa maagizo hayo leo Mei,25,2022 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha kujadili mkataba wa utendaji na utekelezaji wa shughuli za lishe hapa nchini,mkataba uliosainiwa rasmi mwaka 2017 na kuanza kufanya kazi Januari 2018.

Hivyo,Prof.Shemdoe amesema haiwezekani kusubiri mpaka kikao kingine ndipo mpango uanze kutekelezwa kwa sababu masuala ya lishe ni nyeti katika kuhakikisha kila mtoto anakuwa na lishe bora ili kuepuka udumavu.

Katika hatua nyingine Prof.Shemdoe ameanisha maeneo ambayo bado halmashauri hazifanyi vizuri katika utekelezaji ikiwa ni pamoja na eneo la Vitamin A,na Shilingi 1000 kutopelekwa kwa kila mtoto kwa ajili ya utekelezaji wa masuala ya lishe na hilo ndilo aliloliwekea msisitizo mkubwa kuwa maafisa lishe na Wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha fedha hizo zinakuwepo kwa ajili ya kusaidia kupunguza masuala ya utapiamlo nchini

"Natoa maagizo kwa wakurugenzi wote wa halmashauri nchini kuhakikisha wanapeleka fedha za lishe ya kila mtoto shilingi 1000 ili kusaidia kupunguza utapiamlo nchini kuna baadhi ya halmashauri ya Miji hawajapeleka hata pesa kidogo ikiwemo
,Bukombe,Iramba,Serengeti,Musoma Mji,KigomaDC,Tarime,Momba na Mkinga DC hawa naomba ndani ya mwezi mmoja wawe wamekwishapeleka fedha na hii ni kabla ya kuanza mwaka mpya wa fedha wa 2022/2023" Asema Prof.Shemdoe

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Maafisa lishe wa mikoa Benson Sanga amesema wapo tayari kutekeleza maelekezo hayo na wameyapokea na hivyomwatahakikisha maazimio yote watakayotoka nayo katika kikao hicho yanafanyiwa kazi kwa wakati ili kuendelea kutatua changamoto ya masuala ya lishe.

Naye Mkurugenzi Msaidizi huduma za lishe Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mwita Waibe amesema tafiti zinaonesha kuwa mikoa yenye uzalishaji mkubwa wa chakula kwa wingi kama vile mikoa ya Ruvuma,Mbeya ,Rukwa,Songwe na Njombe ndio yenye kiwango kikubwa cha watoto wenye udumavu huku mkoa wa Njombe unaongoza kwa udumavu kwa asilimia 30% ambapo ni wastani wa kitaifa.




No comments:

Post a Comment