Na Okuly Julius-Dodoma
Makamu wa Kwanza wa Rais - Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman amesema Serikali zote mbili zitaendeleaa kuwekeza katika kusaidia ubunifu na matumizi ya teknolojia ili Tanzania iweze kupiga hatua za kiuchumi na maendeleo.
Mheshimiwa Othman amebainisha hayo wakati Uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania inayojumuisha Maonesho ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu - MAKISATU 2022, yanayofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma .
Akikagua bunifu mbali mbali kwenye mabanda ya washiriki wa Maonesho ya Ubunifu Mhe.Othman amesema wabunifu chipukizi ni hazina ya kesho na kusema Taifa litaendelea kukuza vipaji vyao kupitia programu atamizi zinaoratibiwa na kulelewa na tume ya sayansi na teknolojia (COSTECH).
Amebainisha tafiti zaidi kuhusu bunifu katika nyanja za teknolojia na maendeleo hazina budi kupewa umuhimu unaostahili ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kuzalisha bidhaa bora.
Ameishukuru serikali kwa ushirikiano mzunri na shirika la umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo (UNDP) kwa kuendelea kudhamini maonesho ya ubunifu ambapo bunifu nyingi sasazipo kwenye hatua ya kubidhaishwa na zingine mpya zimeibuliwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment