MHE.OTHMAN-MAENDELEO YA UHURU WA HABARI YANAYOONEKANA HIVI SASA DUNIANI NI MATUNDA YA WAANDISHI WENYEWE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 22, 2022

MHE.OTHMAN-MAENDELEO YA UHURU WA HABARI YANAYOONEKANA HIVI SASA DUNIANI NI MATUNDA YA WAANDISHI WENYEWE




Na Mwandishi wetu-Zanzibar

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman amesema kuwa maendeleo ya uhuru wa habari yanayoonekana hivi sasa Duniani, ni matunda ya waandishi wenyewe kuonesha ubora wao na hivyo kutokuruhusu kuyumbishwa, hasa na wenye mamlaka ambao wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi.

Ameyasema hayo hii leo Visiwani Zanzibar wakati akitoa hutuba katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na kuongeza kuwa vyombo vya habari vikisimamia vyema misingi ya habari siyo rahisi viongozi kukiuka maadili na wakaachiwa pasi na hatua zinazo stahiki na huo ndio uwajibikaji wa kweli; Kiongozi awajibike kwa wananchi na asiwe juu ya sheria

"Kwa mnasaba huo, napenda niwakumbushe jambo la msingi ambalo ni kufuata maadili na miongozo ya taaluma yenu ikiwemo kuweka uwiano wa habari, kusikia sauti tofauti, kukaa katika mstari na ushahidi, ili isije ikatokea kinyume chake kama yale yaliyojiri katika Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambapo waandishi walidaiwa kuhusika katika kuhamasisha vurugu" Amesema Mhe.Othman

Pamoja na hayo Mhe.Othman amewataka Waandishi wa habari kujiongezea elimu na maarifa wakitambua kwamba hiyo ndio misingi muhimu ya kujenga ufanisi wa kazi zao na thamani yao kwa jamii hasa katika mazingira ya sasa ya kidigitali;

Pia ni vyema kuwekaza azma ya kuzalisha habari ambazo mnazitafuta weyewe na siyo kutegemea kwa kiasi kikubwa taarifa za kudandia, maarufu kama habari za matukio.

"Tukiri kuwa bado kada ya habari imejikita zaidi katika kuandika taarifa za mijini na kwa uchache habari za vijijini; Hivyo kuna haja ya kubadilika na kutoa nafasi kwa habari za vijijini ili angalau kusaidia katika kuibua kero za wananchi na kusikia sauti zao"Amesema

Mhe.Othman ameongeza kuwa Vyombo vya habari vinapaswa kuibua sauti za watu ambao hawana sauti; pamoja na kuwepo kwa sauti za makundi ya pembezoni wakiwemo wanawake, walemavu, wananchi wa kawaida na wanyonge,Makundi hayo ni yenye mahitaji maalum kwa hivyo ni wajibu kuyasikiliza ili nayo yaweze kupiga hatua. Ukiandika habari bila ya sauti zao, wengi wao hawatoweza kubaini mahitaji yao halisi na kwamba lile duara la kujirejea, la umasikini na unyonge litaendelea kuongezeka.

Pia amewataka kuripoti Habari za Mazingira katika Nchi yetu ni la umuhimu wa pekee, hasa kwa kuzingatia kwamba tumezungukwa na bahari, ambayo ni tishio kubwa la ardhi, kilimo na makaazi ya watu, sambamba na nafasi yake katika utalii. Mambo hayo yote yanaguswa na athari za mabadiliko ya tabianchi (climate change) kuhusiana pia na haiba ya nchi yetu na uchumi wake kwa ujumla.

Ujumbe wa  mwaka huu wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani ni  UANDISHI WA HABARI NA CHANGAMOTO ZA KIDIGITALI.  

No comments:

Post a Comment