Na WyEST
Akiwa katika Chuo hicho Waziri Mkenda amefanya mazungumzo na uongozi wa wa Juu wa Chuo hicho na kukubaliana kuwa na Makubaliano maalum (MoU) ya kuwezesha kuanza kubadilishana uzoefu watumishi wa Chuo hicho na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) pamoja na kuanza kutoa ufadhili (scholarship) kwa wanafunzi wa kitanzania katika eneo hilo.
Aidha Prof. MKenda amefurahi kukutana na wanachuo wawili wa kitanzania William Lohay na Azaria Chongeri wanaosoma chuoni hapo ambao ni watumishi wa DIT kampasi ya Mwanza. DIT kampasi ya Mwanza ni mahsusi kwa eneo la tenolojia ya mazao ya ngozi .
Waziri Mkenda yuko nchini uingezera ambapo anahudhuria kongamano lwa Mwaka la kimataifa la Elimu. *World Education Forum 2022.*
No comments:
Post a Comment