Katika orodha hiyo pia wametajwa, Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Rais wa China, Xi Jinping, Rais wa Kamisheni ya Ulaya (EU) Ursula Von Der Leyen na Kasela wa Ujerumani, Olaf Scholz.
NA ELLEN JOHSON SIRLEAF
Rais Samia Suluhu Hassan aliingia madarakanai mwezi Machi, 2021, na uongozi wake umekuwa tonic. Mwaka huo ulileta tofauti kubwa Tanzania. Mlango umefunguliwa kwa majadiliano na vyama vya upinzani, hatua ambayo imechukuliwa kuwa Ina lenga kujenga kuaminiana katika mfumo wa kisiasa, Hatua zimechukuliwa kuongeza uhuru wa habari na Wanawake na wasichana wamepata kiigizo kipya.
Mwezi September, 2021 miezi michache katika urasi wake, Rais Samia alitoa hotuba kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuandika historia ya kuwa Kiongozi wa Tano mwanamke kulihutubia Baraza hilo. Alisoma katika eneo nililosimama miaka 15 kabla kama Rais wa kwanza niliyechaguliwa kidemokrasia.
"Kama Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi yangu," alisema, "mzigo wa matarajio ya kuleta usawa wa kijinsia ni mzito zaidi kwenye mabega yangu."
Kama alivyosemma maneno haya mazito, sikusaidia ila nilifikiri jinsi mabega ya Kiongozi mwanamama yalivyo madhubuti na kwa jinsi gani wanaweza kuleta tofauti.
Ellen Jonson Sirleaf, ni Rais wa zamani wa Liberia na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel.
No comments:
Post a Comment