Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kimewataka wanafunzi kuchangamkia fursa - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 13, 2022

Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kimewataka wanafunzi kuchangamkia fursa


Na Okuly Julius Dodoma

AFISA Uhusiano wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto mkoani Shinyanga,Josephine Charles ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa za kujiunga na masomo yanayotolewa katika chuo hicho ili kuongeza ujuzi na kupanua wigo wa kujiajiri ama kuajiria katika sekta za afya.

Akizungumza katika maonesho ya vyuo vya ufundi na ufundi stadi yaliyokamilika leo katika viwanja vya jamhri jijini Dodoma amesema katika chuo hicho kinatoa mafunzo mbalimbali ya ufundi pamoja na afya ikiwemo,utabibu,uuguzi na famasia na maabara hivyo kuna fursa kubwa kwa vijana kujiunga na chuo hicho katika kuongeza wigo wa taaluma sekta ya afya.

amesem“Katika chuo chetu kuna program mbalimbali ikiwemo program ya utabibu,program ya uuguzi ambayo ni ya muda mrefu ina Zaidi ya miaka 60,pia tuna program ya maabara ya binadamu na katika chuo chetu tumekuwa tukifundisha kwa vitendo Zaidi na hapa tumeleta baadhi ya dawa ambazo hutengenezwa “amesema Josephine

Aidha,amesema katika program ya uuguzi wamekuwa na vifaa madhubuti ikiwemo baadhi ya vifaa vinavyoonesha namna ya kumsaidia mama anayejifungua.

Mbali na mafunzo ya afya yanayotolewa katika chuo hicho pia kina masomo yanayohusiana na mafunzo ya ufundi stadi[VETA].




No comments:

Post a Comment