Na Okuly Julius-Dodoma
SERIKALI kwa kushirikaina na Umoja wa Taasisi na Vyuo vya Canada wameandaa Programu ya Kukuza Ujuzi wa Kujiajiri kwa wasichana waliokatisha masomo itakayofanyika kwa kipindi cha miaka saba hapa nchini.
Program hiyo itachangia na kuimarisha maeneo ya elimu ya kujiajiri na kuajiriwa, ujasiriamali kwa wasichana na wanawake.
Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku 4 ya Washirika na Wadau muhimu wa ESP - Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs),Asasi za Kijamii (CBOs),Maafisa Maendeleo ya Jamii(CDOš), na MoEST / DTVÉT leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na mafunzo ya fundi stadi kutoka wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Margaret Mussai amesema Programu hiyo imewekeza kiasi cha Shilingi bilioni 45.4 zitakazotumika kuzijengea uwezo FDC 12 na CBO 12 katika maeneo mbalimbali
Aidha, kwa kufanya kazi na FDC na CBOs katiak FDC 12, programu hii inadhamiria kuongeza kiwango cha ushiriki wa wasichana na wanawake katika mafunzo ya kukuza ujuzi na biashara, jinsia na haki za binadamu katika jamii.
"Programu hii ni muhimu sana kwa taifa letu kwani itatusaidia Kuandaa na kutoa mafunzo ya ujuzi ya muda mfupi, walengwa wakuu wakiwa ni wasichana na wanawake720. Aidha, kupitia CBOs wanawake 480 katika jamii watafikiwa na kupata elimu hiyo,Kutoa mafunzo ya Jinsia na haki za binadamu kwa walimu na watumishi 180 kati yao wanawake 60 na wanafunzi 3,200 (Ke 1,000)"Amesema Margaret Mussai
Nakuongeza kuwa "Kuzishirikisha jamii katika shughuli za uhamasishaji na uelimishaji kutambua faida za msichana kujiendeleza kimasomo na kumpa nafasi mwanamke kushiriki mafunzo ya kujenga na kukuza ujuzi ili kujikomboa kiuchumi Wanajamii 2,400 (Ke 1,200) na wanachi watakaojitolea (Volunteers) 36(Ke24) watanufaika na mafunzo haya,"
Mussai amesema kuwa Matokeo mazuri ya Programu hii yatatoa fursa kuwa na mikutano itakayowezesha kubadilishana uzoefu kwa kile jamii ilichojifunza na kupanua wigo kwani Washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya nchi watakutanishwa kuelimishana matokeo na faida ya utekelezaji wa programu ili kuchukuwa yale yenye manufaa na kwenda kuingiza katika afua zao.
Kwa upande wake Meneja wa Programu ya ESP Ndugu Tom Tunney amesema kuwa ni vyema kuunga mkono programu hiyo mpya inayolenga masuala ya kijinsia nchini Tanzania kupitia Mradi wa “Uwezeshaji kupitia Ujuzi”. Programu hii hii inatoa fursa muhimu kwa Muungano wa Vyuo na Taasisi Kanada (CICan) - na taasisi wanachama kuimarisha zaidi ushirikiano wa kitaifa na kimataifa katika maeneo muhimu ya elimu, usawa wa kijinsia, haki za binadamu, mazingira, na ukuaji wa uchumi ambao unahusu kila mtu.
" Nchini Kanada, utaalamu wa wanachama wetu unachangia kupunguza
umaskini na ukosefu wa usawa, hasa kwa wanawake, vijana na watu wasiojiweza, kwa kubadilisha mifumo ya elimu baada ya kumaliza sekondari na kutoa mafunzo yanayolenga ajira",Amesema Ndugu Tom Tunney
No comments:
Post a Comment