HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM YAFANYA UTEUZI WA WAGOMBEA,STEPHEN WASSIRA NAE YUMO - OKULY BLOG

Breaking

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA | PIGA 0785 364 965

Wednesday, June 22, 2022

HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM YAFANYA UTEUZI WA WAGOMBEA,STEPHEN WASSIRA NAE YUMO


Na Okuly Julius-Dodoma

Kamati kuu ya halmashuri kuu ya Chama Cha Mapinduzi, imefanya uteuzi wa wagombea wa nafasi za uenyeviti wa halmashauri ya mji wa Njombe, halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 22,2022 Jijini Dodoma Katibu wa NEC, itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi SHAKA HAMDU SHAKA, amewataja walioteuliwa kugombea nafasi za uenyekiti wa halmashauri za wilaya hizo kuwa ni Ndg Erasto B. Mpete atakayegombea katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mji,Ndg Mohamed Festo Bayo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ,

Wengine ni Ndg Stuart Nathaniel Nkinda,Ndg Apaikunda Ayo Naburi,Ndg Zuberi Abdallah Kidumo wote hawa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi

Aidha, kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha Mapinduzi pia imempongeza kwa dhati Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake na maono yake pamoja na udhubutu wake wa kufungua milango ya maridhiano ya kisiasa nchini.

Katika hatua nyingine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi imefanya uteuzi wa wajumbe wawili wa kamati kuu ya chama hicho ambapo imewachagua kwa kura Ndugu Stephen Masatu Wassira na Ndugu Theresia Adriano Mtewele.

Katibu huyo wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi SHAKA HAMDU SHAKA, amezungumzia umuhimu wa uwepo wa katiba mpya nchini, huku chama hicho kikiishauri serikali kuharakisha yale yote yatakayoendelea kuimarisha maridhiano ya kiasisa baina ya chama tawala na vyama vingine vya siasa

Pia halmashauri kuu ya taifa ya chama cha Mapinduzi imempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. HUSSEIN MWINYI.


No comments:

Post a Comment

HABARI KUU KWA SASA

MAWASILIANO YA BARABARA YA DAR - LINDI KUREJEA NDANI YA SAA 72: BASHUNGWA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameeleza kuwa timu ya watalaamu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na Makandarasi itatumia saa 72 (siku ...