
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt. Tausi M. Kida amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, mapema leo katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Mipango jijini Dodoma.
Mazungumzo yao yamegusia mipango mbalimbali ya utekelezaji wa maono ya Dira 2050 hususani utoshelevu wa nishati ya umeme.


No comments:
Post a Comment