![]() |
Maandamano ya wanafunzi walioanzia katika viwanja vya bunge jijini Dodoma kuelekea Nyerere square kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika hii leo juni 16,2022 |
Na Okuly Julius-Dodoma
Dkt.Gwajima ametoa wito huo leo Juni 16,2022 Jijini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambapo imebebwa na kauli mbiu inayoelekeza kuwa “Tuimarishe ulinzi wa Mtoto; Tokomeza Ukatili Dhidi Yake: Jiandae kuhesabiwa”
Amesema kuwa pamoja na jitihada mbalimbali za kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa watoto, ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa ukatili kuchukuliwa hatua kali za kisheria, bado kuna ongezeko la taarifa za vitendo vya ukatili.
"Ni kweli kabisa bado tunaendelea kushuhudia ongezeko la taarifa za vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ubakaji, Ulawiti, Utumikishwaji wa watoto katika ajira hatarishi, Ukeketaji, Ndoa na mimba za utotoni na vitendo vingine vya ukatili" amesema Dkt Gwajima
Na kuongeza kuwa "Mtoto kwa ajili ya usalama wako jiepushe kwenda kwenye maeneo ambayo ni hatari na kuwa karibu na watu usiowafahamu au wanaotaka kuzoea mwili wako; kwa kufanya hivyo utajiepusha na kushawishiwa kufanya ngono au kubakwa, kulawitiwa na hata kuuawa," Dkt.Gwajima
Dkt.Gwajima amesema kwa mujibu wa Takwimu za Jeshi la Polisi, Tanzania katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2021 jumla ya matukio ya ukatili kwa watoto yaliyoripotiwa katika jeshi la Polisi ni 11,499 ikilinganishwa na matukio 15,870 katika kipindi kama hicho mwaka 2020 (upungufu ni matukio 4,371 sawa na asilimia 27.5).
Ambapo Mikoa iliyoongoza ilikuwa ni Arusha (808), Tanga (691), Shinyanga (505), Mwanza (500) na Mkoa wa Kipolisi Ilala (489). Aidha, makosa yaliyoongoza kwa idadi kubwa ni ubakaji (5,899), mimba kwa wanafunzi (1,677) na ulawiti (1,114).
Hata hivyo Kwa upande mwingine, utafiti wa serikali na UNICEF unaonesha asilimia 60 ya matukio yanatokea nyumbani na asilimia 40 yanatokea mashuleni na matukio haya ni yale yalioripotiiwa ila kuna uwezekana kukawepo kwa matukio mengi ambayo hayajaripotiwa.
"kuna uwezekano mkubwa kwamba matukio ya ukatili yanaweza kuwa mengi kuliko haya ukizingatia kwamba haya ni yale tu yaliyotolewa taarifa kwenye vituo vya polisi hivyo nitoe wito kwa jamii kukemea na kuripoti matukio ya kikatili ili kukomesha tabia hii"Amesema Dkt.Gwajima
Aidha Dkt. Gwajima amesema Katika kukabiliana na aina mpya ya Ukatili Dhidi ya Watoto Mitandaoni unaosababishwa na kukua kwa Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Serikali imefanya jitihada kadhaa ikiwemo ,Kuunda kikosi kazi cha taifa cha Ulinzi na Usalama wa Mtoto mtandoni kikiwa na malengo la Kuhakikisha watoto wako salama wakiwa mtandaoni.
"Naomba sasa kusiwe na mtanzania anayelalamika kuhusu ukatili bila kuchukua hatua, bali sasa inuka jiunge na SMAUJATA twende mstari wa mbele kutokomeza ukatili. Nguvu yetu umoja wetu ushindi ni lazima na uko mlangoni, fungua mlango ushindi uingie," Dkt.Gwajima
Pia amewaasa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii katika Mikoa na Halmashauri zote nchini kuimarishautoaji wa elimu ya malezi na makuzi ya watoto kwa wazazi na walezi ili waelewe wajibu wao wa kulea watoto kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa wa kijinsia na kuwaelekeza Wazazi au walezi kuwasimamia watoto wao kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kielektroniki ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika mitandao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara hiyo, Sebastian Kitiku, akitoa maelezo ya mwongozo wa taifa wa baraza la watoto, amesema kuwa unalenga kuwafanya watoto kutoa taarifa za ukatili dhidi yao.
Maadhimisho ya mtoto wa Afrika yalikuja kufuatia kuuawa Zaidi ya watoto 2000 katika kitongoji cha Soweto Afrika Kusini wakati wa maandamano ya kupinga elimu ya kibaguzi dhidi ya watoto wenye asili ya kizungu.
No comments:
Post a Comment