MARUFUKU KUPANGA SAFU ZA UONGOZI KABLA YA WAKATI-CHONGOLO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 16, 2022

MARUFUKU KUPANGA SAFU ZA UONGOZI KABLA YA WAKATI-CHONGOLO


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ametoa onyo kwa Makatibu wa CCM na Jumuiya zake kuacha mara moja kupanga safu za uongozi kabla ya muda kufika .

Hayo ameyasema Juni 15,2022 Jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambapo ameeleza Bajeti hiyo ya serikali imebeba muelekeo wa ukuaji kasi wa kiuchumi na inaelekeza wazi inataka kututoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Amesema anazo taarifa kuwa Makatibu wa chama na jumuiya wanazungushwa kutoka hotel moja kwenda nyingine na kusahau kuwa wao ni wakurugenzi wa uchaguzi.

"Sitamani kuona Makatibu wangu mnajiingiza kwenye ushabiki wa kutafuta na kutengeneza wagombea endapo ukibainika jua kazi huna niwaombe tena Makatibu wa chama na Jumuiya achacheni kubebana bebana kwenye hotel moja kwenda nyingine mnaiabisha jumuiya yetu na kurudisha nyuma chama chetu fanyeni kazi yenu," alisema Chongolo.

Na kuongeza Kusema "Inatia aibu sana Kuna watu wameshajitengenezea wagombea kwa nafasi mbalimbali kumbukeni sisi tupo na ndio viongozi tuliopewa dhamana katiba Kanuni na miongozo halali ya chama chetu hivyo tunaomba msitupatie viongozi kabla ya muda," amesema .

Amesema wagombea wote tutawapata kwa muda na utaratibu bila kuangali sifa za pembeni bali tunaangali sifa za mgombea tunamuangali anaweza kutuombea kura pale anapotumwa aweze kutusemea kutuunganisha Pamoja ajenge uchumi tunataka mtu muonekano wake uendane na Matendo yake yaendane na Hali ya Jumuiya ya (UWT).

Amesema tunataka mtu au kiongozi akisimama Watu waseme mwenye Jumuiya yake amesimama hii ni Jumuiya mama hatutaki Viongozi ambao ni mabingwa wa kukopi sifa za wenzao .

Amesema mtu kutangaza nia wakati ukifika sio dhambi wala kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi sio dhambi ila kuna mambo yanayotaka kujitokeza hayafurahishi kwani watu wako busy tayari wameshajipatia nafasi.

"Mbaya zaidi ni pale tunapoona viongozi wakubwa wameshapewa wagombea Mimi taarifa huwa napewa taarifa juu ya chama chetu na kile kinachoendelea ndani ya chama hivyo ni aibu kuona mtu mzima anatumia jina la kiongozi wake kuwa anatumika na kiongozi wake achukue fomu na kugombea nafasi fulani.

Na kuongeza Kusema "Kiongozi anayedhamilia kuwa kiongozi na anayejiamini haitaji kutumia jina la mwingine ili afanikiwe bali kiongozi anayejiamini anajipima nafasi yake ajithamini vigezo na sifa Ni za kwake na sio sifa za mwingine," alisema .

Amesema kiongozi anayetakiwa ni yule mwenye dhamira ya kutupeleka mbele tumtathimini kwa sifa zake na sio kwa sifa za mtu fulani kwani kiongozi wa mtu fulani hana dhamira njema na chama pia kiongozi wa dhati ni yule anayesimama na miguu yake mwenyewe sio kwa miguu ya mwengine.

Aidha amebainisha ukijipitisha kabla ya muda kufika utakuwa umekiuka taratibu na sisi kama chama tutakukata jina lako kwani umekiuka Kanuni na taratibu.

KUHUSU BAJETI.

Chongolo alisema wanaipokea Bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwani imebeba matumaini ya msingi kwa wanawake na watanzania kwa ujumla huku akiwataka wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania waijadili kwa Makini na kuipitisha kwa maslahi ya chama.

Awali akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka amesema chaguzi za matawi zimepita salama na wanawake wameonekana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali huku akisema chaguzi za matawi zimetoa picha chaguzi zimekwenda vizuri .

Naye Naibu Katibu Mkuu Bara Christina Mndeme amewataka wanawake kuonesha kwa vitendo kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia unaoonekana kushika kasi kwani Jumuiya yetu inahusika katika kuhakikisha tunapinga vikali vitendo hivvyo.

No comments:

Post a Comment