![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika Juni 29,2022 jijini Dodoma. |
![]() |
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika Juni 29,2022 jijini Dodoma. |
Na Okuly Julius Dodoma
SERIKALI imeagiza Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuangalia uwezekano wa kuanzisha mfumo wa kiutawala wa kukusanya taarifa za Hali ya Ulemavu Nchini kama inavyofanyika kwa takwimu za vifo vya watoto wachanga na vifo vinavyotokana na uzazi.
Aidha imewataka watu wenyeulemavu kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi ili serikali ipate takwimu zinazoakisi uhalisia na ambazo zitatumika katika kutunga sera na kupanga mipango na programu mbalimbali za maendeleo ambazo zitazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu
Hayo yameelezwa juni 29,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu George Simbachawene wakati akifungua kongamano la watu wenye ulemavu lililoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Taifa ya takwimu.
Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuyapa kipaumbele na nafasi kubwa masuala ya watu wenye ulemavu kwa kuwajali na kuwathamini.
"Katika kuhakikisha kuwa jamii ya watu wenye ulemavu kama zilivyo jamii nyingine wanakuwa sehemu ya mchakato mzima wa sensa ya watu na makazi, serikali imezingatia ushiriki wao katika hatua zote za utekelezaji wa zoezi hili la kitaifa. Ushiriki wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu nchini (SHIVYAWATA) ni ishara ya ujumuishaji huo.
Ameongeza kuwa "Wameshiriki katika maandalizi ya madodoso na miongozo ya sensa; mafunzo ya makarani na hatimaye katika zoezi zima la Sensa ya Majaribio lililofanyika nchini Agosti 2021; sambamba na kushiriki katika mafunzo na zoezi la kuhesabu watu.
Kwa mujibu wa Simbachawene alisema katika kutekeleza azma ya kuwatumikia watu wenye ulemavu kama sehemu ya watanzania, serikali imeendelea kufufua Vyuo vya Ufundi Stadi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu ambavyo kwa muda mrefu vilikuwa vimefungwa kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa miundombinu ya vyuo.
"Serikali kwa kutambua umuhimu wa mafunzo ya ufundi stadi kwa watu wenye ulemavu imekarabati Chuo cha Luanzari Tabora ambacho kimefunguliwa na kuanza kufanya kazi mnamo Julai, 2021 chenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 120,"alisema
NDERIANANGA
Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Ummy Ndarienanga amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu na kuwaamini katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Amesema watahakikisha wale waliopata nafasi mbalimbali za uongozi watahakikisha wanafanya kazi Kwa bidii ili wasimuangushe Rais Samia na aendelee kuwaamini wengi zaidi kwani wanaweza.
" Nampongeza Rais Samia kwa kutujari sisi wenye ulemavu ameonyesha kutupenda na tunamhakikishia kuwa tutaendelea kumpa ushirikiano tunaomba aeendelee kutuamini na kutoa nafasi mbalimbali za uongozi na sisi tunamhakikishia kuwa hatutamuangusha tutafanya kazi kwa bidii,"amesema
CHUWA
Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa amesema lengo la kuandaa kongamano hilo ni kupeana misingi na faida ya zoezi la sensa ya watu na makazi kwa watu wenye ulemavu.
Amesema tangu maandalizi ya sensa yalipoanza mwaka 2018 serikali ilianza kushirikisha kundi la watu wenye ulemavu katika hatua mbalimbali lengo ni kuhakikisha nao wanahesabiwa na Taifa linakuwa na takwimu sahihi la kundi hilo.
"Katika ya sensa ya watu na makazi ya itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu tumeweka maswali ya kutosha ambayo yatasaidia kupata takwimu sahihi zitakazosaidia serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla,"alisema
Ameongeza kuwa"Hii ni sensa ya sita kufanyika hapa nchini lakini chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itahusisha Kwa kiasi kikubwa watu wenye ulemavu kuliko sensa zilizopita,.
KIMANI
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha watu wenyeulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Diwani Kimani amesema kongamano hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia la kutaka sensa ya watu na makazi ya mwaka huu kushirikisha watu wenye ulemavu.
Amesema kongamano hilo linaenda kufungua uelewa kwa watu wenye ulemavu ili wakahamasishe watu wengine kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi kwa lengo la kupata takwimu sahihi kwa ajili ya mipango ya serikali.
"Tunatarajia baada ya kupata uelewa tutaenda kuhamasisha watu wengine ili wajitokeze kuhesabiwa katika sensa ya mwaka huu na sasa kuna timu ya uhamasishaji inayopita katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar ninaendelea na tumefurahishwa kuona watu wenye ulemavu wameshirikishwa katika timu hiyo na wanafanya kazi nzuri,"amesema
KATAMBI
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana,Ajira,Kazi na Watu wenyeulemavu Patrobas Katambi alisema Rais Samia ametoa kiwanja Mtumba jijini dodoma chenye thamani ya sh.milion 36 Kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya shirikisho la chama Cha watu wenye ulemavu.
Katambi ameongeza kuwa Rais Samia amekuwa akijipambanua katika kujali kundi hili la watu wenye ulemavu Kwa kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha haki zao zinalindwa, kutoa kipambele kwa watu wenye ulemavu katika fursa mbalimbali zinazojitokeza nchini.
Pia ametaja maagizo mengine kuwa ni Kushirikisha kundi hilo katika mambo mbalimbali ya ayohusu yanahu taifa lao, kusimamia masuala ya kuhakikisha haki zao zinalindwa na kuagiza hatua Kali kuchukuliwa Kwa wale wanaobainika kuvunja haki za watu wenye wenye ulemavu.
"Rais Samia alisisitiza pia kuhakikisha watu wenye ulemavu wanawezwashwa kiuchumi Haki katika kuhakikisha wanapata mikopo kwa ajili ya kendesha shughuli mbalimbali za Kilimo, ufugaji na biashara.
Ameongeza Kwa"Elimu jumuishi kuhakikisha ngazi zote watu wenye ulemavu wanapata na Taya katika kuhakikisha hilo tayari Rais Samia ametoa fedha kwa ajili ya kujenga mabweni 50 katika Halmashauri 50 lengo ni kuhakikisha wanapata elimu Bora.
Katambi amesema pia Rais Samia ametoa kiwanja jijini Dar es Salam Kwa ajili ya kujenga ofisi katika Mkoa huo.
MTAKA
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Athony Mtaka amesema mkoa wa Dodoma utahakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao za msingi katika mkoa huo ili kuimarisha ushiriki wao katika zoezi la Sense ya watu na makazi.
“Sisi kama Mkoa wa Dodoma tumeshaanza na tumekuwa na ushirikiano na viongozi wote wa vyama vya Watu wenye ulemavu Mkoa wa Dodoma kwenye shughuli zetu nyingi na kwenye hili tumefanya ushirikiano wa pamoja”amesema
” Mh. Simbachaweni nikuakikishie sisi kama Mkoa wa Dodoma tutatekeleza moja kwa moja maagizo uliyoyatoa siku hii ya leo”.amesema Mtaka
No comments:
Post a Comment