TAASISI NA MAMLAKA ZA UTHIBITI UBORA SAIDIENI KUENDELEZA BUNIFU SIO KUDHIBITI -PROF.MDOE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 21, 2022

TAASISI NA MAMLAKA ZA UTHIBITI UBORA SAIDIENI KUENDELEZA BUNIFU SIO KUDHIBITI -PROF.MDOE

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe Akizungumza leo Juni 21,2022 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau wa Elimu ,Sayansi, teknolojia na Ubunifu iliyoandaliwa na Idara ya Elimu,Sayansi, Teknolojia na ubunifu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe (kushoto) leo Juni 21,2022 jijini Dodoma wakati wa mkutano wa wadau wa Elimu ,Sayansi, teknolojia na Ubunifu iliyoandaliwa na Idara ya Elimu,Sayansi, Teknolojia na ubunifu (kulia) ni Mkurugenzi wa Elimu,Sayansi, teknolojia na ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho kilichokutanisha wadau wa Elimu,Sayansi,teknolojia na ubunifu pamoja na Idara ya Elimu,Sayansi, teknolojia na ubunifu kutoka wizara hiyo.

Na Okuly Julius Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe ametoa wito kwa taasisi na mamlaka za uthibiti ubora hapa nchini kufanya kazi kwa kuhamasisha ubunifu na kuendeleza wabunifu  na sio kuwadhibiti.

Kwa kufanya hivyo utasaidia kuinua na kuendeleza bunifu badala ya kuzuia bila kutoa njia nzuri ya kuendeleza bunifu kwani wabunifu wengi wamekuwa wakikata tamaa baana ya kufika katika hatua ya kwenda kupitishwa na kuthibitishwa kwa mamlaka husika na hapo ndipo ugumu unapoanza kutokana na Sheria zilizopo.

Akizungumza leo Juni 21,2022 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau wa Elimu ,Sayansi, teknolojia na Ubunifu iliyoandaliwa na Idara ya Elimu,Sayansi, Teknolojia na ubunifu Prof.Mdoe amesema kuwa bunifu mbalimnali zimekuwa zikikwamishwa na mamlaka hizi za Uthibiti ubora kutokana na kuacha lile lengo lao la msingi la kuthibiti na kuamua kudhibiti jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma wabunifu hapa nchini

"Ujumbe wangu ninaoupeleka kwa Regulators tena leo nafamu kwa asili ya sheria zilizounda taasisi hizi za Uthibiti ubora zimekaa kipolisipolisi na hazihamasishi ubunifu kwa hivyo kama mtu akija na kitu chake amekibuni yaani kitu cha kwanza anaulizwa Una leseni? Umelipia? Lakini huyo ndio kwanza anakibuni hajajua hata kinafanyaje kazi alafu wewe unamwambia habari za leseni wakati hata hajatesti hiyo ni kurudisha nyuma bunifu zetu fanyeni kazi yenu ya kuthibiti ubora na sio kudhibiti ishini  kwa kuzingatia tofauti ya haya maneno mawili mtusaidia kuendeleza bunifu na sio kurudisha nyuma" amesema Prof. Mdoe

Na kuongeza kuwa "Mtu anabuni kitu chake wewe unakuja kudhibiti ujue tu kuwa kazi yenu ni kuFacilitates sio kuzuia mjitahidi kufanya kazi yenu maana sisi ni mamlaka ya kuthibiti ubora kwa sababu kama waratibu wa Masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu tunafanya kazi bure kama nyinyi mnashindwa kuendeleza bunifu na badala yake mnadhibiti mtambue tu kuwa mnarudisha nyuma wabunifu na nchi kwa ujumla"

Aidha Prof.Mdoe ametaka Idara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na ubunifu pamoja na wadau mbali na kazi kubwa waliyonayo ya kujadili Muongozi bado mnakazi kubwa ya kuutambua na kuuendeleza hivyo kazi kubwa ya kuuendeleza upo katika taasisi za kuthibiti.

Prof.Mdoe amesema kuwa matarajio yake makubwa kupitia kikao kazi hicho watakuja na Muongozo mzuri ambao utaleta matokeo makubwa katika kuibua wabunifu wapya kuliko huko nyuma na muongozo ambao utakuwa shirikishi kwa upande wa serikali pamoja na sekta binafsi nazo ziwe na uwezo wa kuendeleza bunifu hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu,Sayansi,teknolojoa na ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula amesema kuwa idara ya elimu,sayansi,teknolojia na ubunifu kwa kushirikiana na wadau wa elimu ina kazi kubwa sana ya kupitia na kuendeleza Miongozo mbalimbali hasa inayoshughulikia masuala ya ubunifu kwani nchi ili iendelee ni lazimu sayansi ,teknolojia na ubunifu ipewe kipaumbele hasa katika kuhakikisha bunifu zinazobuniwa na Watanzania zinaendelezwa na kubiasharishwa ili iweze kuleta matokeo chanya kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja.

No comments:

Post a Comment