Na Okuly Julius-Dodoma
Akizungumza katika kongamano la wenye Ulemavu lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya taifa ya takwimu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga amesema kuwa timu ya wenye ulemavu kuna siku italeta kombe la Dunia hapa nchini na hiyo itaendelea kuwa heshima kubwa kwa taifa.
"Timu ya wenye ulemavu tutaendelea kuipeperusha bendera ya taifa na tunaahidi tutabeba kombe la dunia na itajivunia hii timu sana" Amesema Ummy Nderiananga
Pia ameiomba serikali kuwepo kwa bonanza maalumu la kuibua vipaji vya watu wenye ulemavu kwa kufanya hivyo kutaibua vipaji vingi vilivyojificha kwa walemavu huku akitoa mfano kwa mshindi wa BSS Msimu ulioshi kuwa ni mlemavu na ameibuka mshindi hivyo kuonesha kuwa walemavu wana vipaji vikubwa.
"Mhe.Mgeni rasmi nina furaha sana kwasababu swala hili nimelipendekeza hapa na wewe utalifanyia kazi lifika mahala husika kwa sababu najua bonanza maalumu la wenye ulemavu itatusaidia kuibua vipaji vilivyopo ndani yao"amesisitiza Nderiananga
Aidha amewataka kuwa mabalozi wakubwa katika zoezi la Sensa ambalo linatarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu hivyo watumie fursa hiyo kuhamasisha jamii kujitokeza kuhesabiwa.
Kauli mbiu katika Kongamano hilo imebebwa na kauli isemayo "sisi watu wenye ulemavu tutashiriki kuhesabiwa katika Sensa tarehe 23 Agosti, 2022"
No comments:
Post a Comment