WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI WA DARAJA LA KATUMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 14, 2026

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI WA DARAJA LA KATUMA


Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa daraja la Katuma mita 55 katika barabara ya Sitalike-Kizi km 64.

Akizungumza mara baada ya kuikagua barabara hiyo ameipongeza Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kwa kazi nzuri.

Nae Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema daraja hilo lililogharimu shilingi bilioni 9.1 litaondoa adha kwa wananchi kuvuka mto Katuma na kuunganisha kwa njia fupi mkoa wa Katavi na Rukwa kupitia hifadhi ya taifa ya Katavi.

Ujenzi wa daraja la Katuma ni muendelezo wa mkakati wa Serikali kujenga madaraja ya kudumu sehemu ambazo huathiriwa mara kwa mara wakati wa mvua nyingi na kuleta kero kwa wananchi.

Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Kibaoni- Sitalike km72 na mipango ni kuijenga barabara ya Kibaoni- Majimoto hadi Inyonga km 162 ili kuuunganisha kwa njia fupi mkoa wa Tabora, Katavi na Rukwa.



No comments:

Post a Comment