Na WMJJWM-New York Marekani
Tanzania imeshiriki Mkutano wa masuala ya Jinsia na Wanawake wa nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kando ya Mkutano wa 70 wa Hali ya Wanawake Duniani unaendelea jijini New York nchini Marekani kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali yaliyokubaliwa kutekelezwa katika Mkutano huo kwa mwaka 2026.
Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Barke Sehel kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi wengine waliohudhuria ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Felister Mdemu na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara Eveline Makala.
Wakati huo huo Tanzania imeshiriki katika Mkutano na Shirika la Umoja wa Mataifa linaliloshugulikia masuala ya Wanawake (UN Women).
Mkutano wa 70 wa Hali ya Wanawake Duniani unaendelea jijini New York nchini Marekani unalenga kuzikutanisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kujadiliana masuala ya maendeleo ya Wanawake ukiwa na Kaulimbiu isemayo:"Kuhakikisha na Kuimarisha upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Wasichana wote, ikiwa ni pamoja na kukuza mifumo ya kisheria nyenye usawa na jumuishi, kuondoa sheria, sera, na desturi za kibaguzi na kushughulikia vikwazo vya kimuundo".







No comments:
Post a Comment