MAFUNZO YA KITAIFA YA USALAMA DHIDI YA MIONZI YAFUNGWA RASMI BUZWAGI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 14, 2026

MAFUNZO YA KITAIFA YA USALAMA DHIDI YA MIONZI YAFUNGWA RASMI BUZWAGI


Mafunzo ya Kitaifa ya Ulinzi na Usalama Dhidi ya Mionzi kwa Watumiaji wa Vifaa vya X-Ray Fluorescence (XRF) yaliyofanyika Buzwagi kuanzia tarehe 10 Machi 2026 yamehitimishwa rasmi Jumamosi, tarehe 14 Machi 2026. Sherehe ya kufunga mafunzo hayo iliongozwa na Mkuu wa Ofisi ya Tume Kanda ya Ziwa, Dkt. Suleiman Ameir Suleiman, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Prof. Najat Kassim.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo, Dkt. Suleiman aliwapongeza washiriki kwa ushiriki wao wa dhati katika nadharia na vitendo, na kusisitiza kuwa maarifa waliyopata ni nyenzo muhimu kwa usalama wao binafsi, taasisi wanazofanyia kazi, na Taifa kwa ujumla.

Alieleza kuwa teknolojia ya XRF imekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya madini na viwanda kwa kubaini muundo wa elementi za kemikali, lakini pia inaleta changamoto za kiafya endapo haitatumika kwa kuzingatia kanuni za usalama.

Washiriki walipewa maelekezo ya kuzingatia mambo yafuatayo baada ya mafunzo:
Kutumia maarifa ya misingi ya mionzi na athari zake kiafya kwa kuimarisha usalama kazini, Kufuata kanuni za ulinzi na usalama dhidi ya mionzi kwa mujibu wa Sheria ya Nguvu za Atomu, Sura ya 188, Kupunguza dozi ya mionzi kwa wafanyakazi kwa kutumia mbinu walizojifunza, Kutumia vifaa vya ufuatiliaji wa mionzi kwa usahihi na kwa wakati na Kuzingatia taratibu za kazi salama na kuwa tayari kuchukua hatua za dharura endapo hatari itatokea.

Aidha, washiriki walihimizwa kutumia maarifa hayo kwa manufaa ya taasisi zao na kushirikiana na TAEC katika kuhakikisha viwango vya kitaifa na kimataifa vya usalama wa mionzi vinafuatwa.

Dkt. Suleiman aliwashukuru waandaaji wa mafunzo pamoja na wakufunzi kwa juhudi zao kubwa, na kupongeza uongozi wa Bulyahulu kwa ushirikiano wao katika kufanikisha kozi hiyo muhimu.


Mafunzo haya yamehitimishwa kwa mafanikio na yanatarajiwa kuimarisha utamaduni wa usalama kazini, kulinda afya za watumiaji wa teknolojia ya XRF na jamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment