Na Okuly Julius Dodoma
KATIBU mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael amesema kuwa atawasiliana na wizara ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kupata maeneo ambayo yanahitajika kuweka mkazo mkubwa katika kuhakikisha wanafunzi wanasoma kada hiyo ili kupunguza uhitaji uliopo .
Amesema hayo wakati alipokaribishwa kwa mara ya kwanza kama katibu mkuu wa wizara hiyo mtumba jijini dodoma huku akiahidi kuwa atafuata miongozo na yale mazuri yaliyokuwa yanaendelezwa na watangulizi wake.
"Mimi kama katibu mkuu nitapita kwenye mipango na malengo ya wizara ili kuhakikisha sitoki nje ya malengo yaliyopo na mnaona hivi karibuni tu Rais wetu Mhe.Samia amepitisha Elimu bure kwa kidato cha tano na sita kikubwa ni kulinda maono na ile ndoto njema ili kuifikisha Elimu ya Tanzania katika eneo salama "Amesema Dkt.Franci Michael
Pia Dkt.Francis amesema kuwa amelengwa na mambo mengi yakiwepo ya kufanya mapitio ya mitaala ambapo ndilo suala lilipo kwa sasa huku akibainisha kuwa mambo yote yatakayofanyika katika ofisi yake itazingatia zaidi Bajeti ya wizara hiyo ambapo ndio itakuwa muongozo mkuu kwa upande wake ili kuendelea kuboresha elimu hapa nchini.
Ameahidi ushirikiano mkubwa kwa watendaji wa wizara hiyo huku akibainisha kuwa kwa sasa amepelekwa eneo ambalo anajisikia yupo nyumbani kwani kitaaluma yeye ni mwalimu na anajua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu hivyo kwa kushirikiana na watendaji wote anaamini kuwa watafikia malengo huku akiwataka kila mmoja afanye kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kumsaidia Rais kutimiza maono yake.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amemhakikishia ushirikiano mkubwa katibu huyo Mpya huku akisema kuwa watendaji wa wizara hiyo ni wachapa kazi hivyo atafurahia uwepo wake ndani ya timu hiyo mpya.
"Nakuhakikishia kuwa hapa ulipokuja ni kama nyumbani kwako na hawa unaowaona mbele yako ni majembe kweli kweli naongea hivyo nikiwa na uhakika mkubwa kuwa utafurahia uwepo wako hapa lakini naomba usituchoke sisi kuna muda tutahitaji documents naomba utusaidie kwa sababu ni katika hali ya kufanya mambo yakae sawa sawa" Amesema Omary Kipanga
No comments:
Post a Comment