WADAU WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KUHUSU TAARIFA ZA MMILIKI MANUFAA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 3, 2022

WADAU WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KUHUSU TAARIFA ZA MMILIKI MANUFAA


Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara wa BRELA, Bw. Meinrad Rweyemamu akizungumza katika Warsha hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Amina Makilagi akifungua warsha hiyo

Na Mwandishi wetu Mwanza 

Wakala Wa Usajili Wa Biashara na Leseni (BRELA), imetoa wito kwa wadau kutoa elimu kuhusu dhana ya Mmliki Manufa katika kampuni, Ili taarifa hizo zipatikane kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika warsha ya siku mbili kuhusu uhamasishaji wa wadau kutoa taarifa hizo inayo fanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Benki Kuu Jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara, Bw. Meinrad Rweyemamu amesema kuwa taarifa hizi zinapaswa kuwasilishwa kwa mujibu wa Sheria Ili kupata taarifa muhumu na sahihi za mmiliki halali wa kampuni.

"Kuna baadhi ya wamiliki wa
kampuni wanaonekana katika mfumo Ila katika uhalisia siyo wamiliki halali, hivyo ni vyema taarifa hizi zikawakilishwa kwa Msajili Ili Mmliki Manufaa atambulike, kwani kuna uwezekano mkubwa kuwa mtu anamiliki kampuni lakini hataki kujulikana, hivyo taarifa hizi zitasaidia kumjua Mmliki Manufaa ni nani katika kampuni," amefafanua Bw. Rweyemamu.

Ameongeza kuwa taarifa hizi za Mmiliki Manufaa zinatakiwa Ili pia kumfahamu mtoa maamuzi katika kampuni kwa lengo la kupunguza mianya ya utakatishaji fedha na kutambua vyanzo vya fedha vya wamiliki wa kampuni kwa usalama wa Taifa na uchumi kwa Ujumla.

“Dhana hii ni nzuri na ni lazima ifahamike kwa wadau na wamiliki wa kampuni, kwani inatoa wigo kwa Serikali kufanya maamuzi sahihi kama kuzuia masuala ya utakatishaji fedha, rushwa, kupanga kodi, pamoja na kuzuia mianya ya ugaidi, Dunia nzima inaelekea huko, hatuna budi kuelekea huko," Amesema Bw. Rweyemamu.

Ameongeza kuwa awali mfumo ulikuwa unapokea taarifa bila kujali kinachofanyika, mtaji unatoka wapi, hivyo Suala hili likawa chanzo cha mianya ya rushwa na tishio la kiusalama, ndiyo maana Sheria ya kuzuia utakatishaji fedha ikapitishwa hivyo, kampuni zikatakiwa kuwasilisha taarifa za Wamiliki Manufaa ili ifahamike chanzo cha fedha wanazomiliki.

Ameowaomba wadau walioshiriki warsha wakiwemo Mawakili na Wawakilishi wa wamiliki wa kampuni kutoa mwanga kwa wadau wengine Ili dhana hiyo iwe yenye kujenga taifa la Tanzania.

Awali akitoa hutuba ya ufunguzi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Amina Makilagi amewapongeza wadau kujitokeza kwa wingi na kuomba waendelee kutoa ushirikiano kwa BRELA ili Kufanikisha dhana nzima ya urasimishaji biashara nchini.

 Pia ameongeza kuwa taarifa za Wamiliki Manufaa zinapaswa kuwasilishwa kwa wakati kwani muda wa uwasilishaji uliongezwa na Serikali hadi Juni 30, 2022, Ili kufanikisha suala hilo.

 Hata hivyo ameitaka BRELA kuendelea kutoa elimu hiyo ili kuwafikia wamiliki wa kampuni wengi zaidi.

No comments:

Post a Comment