Serikali inayoongozwa na Rais
Samia Suluhu Hassan imetenga
eneo lenye ukubwa wa kilomita za
mraba 2,500 lililopo kwenye Pori
Tengefu la Loliondo kwa ajili ya
makazi ya wananchi.
Hayo yameelezwa huko
Loliondo mkoani Arusha na Mkuu
wa Mkoa huo, Mhe. John Mongella alipotembelea eneo hilo.
“Uongozi wa mkoa, uongozi wa
wilaya na vyombo vyetu vya ulinzi
na usalama tupo Loliondo, hali ni
shwari na kama mnavyojua
tunaendelea na zoezi la kuweka
mipaka kwenye eneo la pori
tengefu la Loliondo ambalo lina
kilomita za mraba 1,500.
“Na kama mtakumbuka kuwa kwa
mujibu wa sheria eneo ambalo ni
pori tengefu ni kilomita za mraba
4,000 lakini Serikali kwa makusudi
kabisa kwa kujali shughuli za
wananchi sasa imetenga kilomita
za mraba 2,500 kwa ajili ya wananchi kuendelea na shughuli zao.
“Na kilomita 1,500 za mraba kwa
ajili ya uhifadhi wa eneo nyeti la
mazalia ya wanayama, njia zao na
vyanzo vya maji, eneo hilo ndio
chanzo kikuu cha maji kwenye
Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro
na Hifadhi ya Masai Mara iliyopo
Kenya,” ameeleza Mkuu wa Mkoa. |
No comments:
Post a Comment