Na Mwandishi wetu Dar-es-salaam
Hayo yamebainishwa leo tarehe 28 June, 2022 na Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Happiness Mbelle alipokuwa akifungua mafunzo kwa wafanyabiashara 41 wa mbolea yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Kilimo ofisi ndogo ya wizara Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mbelle ameeleza kuwa biashara ya mbolea inamtaka mfanyabiashara wa mbolea kupata mafunzo na kutunukiwa cheti kitakachowekwa dukani kwake ili kurahisisha mchakato wa udhibiti unaofanywa na mamlaka.
“Mkifanya biashara ya mbolea mzingatie sheria, kanuni na taratibu za kujihusisha na biashara ili kuepuka changamoto za kufutiwa leseni na kufungiwa maduka yenu.
Aidha, Mbelle amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu na kutosita kuuliza jambo lolote litakalohitaji ufafanuzi kutoka kwa wataalamu wa mamlaka.
"Muwe huru kuuliza ili mpate uelewa wa kutosha katika kujihusisha na biashara hii ili kuifanya kwa weledi na ufanisi” amesisitiza Mbelle.
Akitoa mafunzo kwa wafanyabiashara hao, Afisa Udhibiti Ubora kutoka TFRA Gema Nganyagwa, amewashauri wamiliki wa maduka na maghala ya mbolea kuwawezesha watendaji katika vituo vyao ili wapate elimu ya mbolea ambapo baada ya mafunzo watatunukiwa vyeti vitakavyopaswa kuwekwa kwenye maduka yao kuonesha uhalali wa kuuza bidhaa hiyo.
“Tusifanye maisha marahisi kwa kukwepa sheria, tusiwe wabinafsi tuwalete wanaotufanyia kazi waweze kushiriki kwenye mafunzo ili waweze kufanya kazi kwa weledi” amesisitiza N.ganyagwa
Kama taasisi tunatamani wafanyabiashara mpate mafunzo ili tunapopita kukagua na kuamua kuchukua sheria isiwe kama mnaonewa na ndio maana tunaandaa mafunzo haya mara kwa mara kuondoa visingizio.
Kwa upande wake mmoja wa wafanyabiashara Isabela Mwatebela kutoka ameiomba Mamlaka kuwasaidia namna ya kuwapata wauzaji wenye taaluma ya masuala ya mbolea kutokana na changamoto ya wauzaji hao kutotumika muda mrefu sehemu moja.
Akijibu ombi hilo Afisa Udhibiti Ubora Schola Mbalila na mtoa mada kwenye mafunzo hayo amesema taasisi inawasaidia wafanyabiashara hao kwa kuratibu na kutoa mafunzo mara kwa mara na kuwasisitiza kuwawezesha wauzaji wa mbolea kushiriki kwenye mafunzo hayo yanayotolewa bila gharama yeyote.
No comments:
Post a Comment