
Kampuni ya mabasi ya Shabiby Bus imefanya maboresho makubwa ya vyoo katika Kituo Kikuu cha Upakiaji Abiria jijini Dodoma, vilivyokuwa katika hali ya uchakavu, hatua inayolenga kuboresha mazingira na ustawi wa wasafiri.
Mbali na maboresho hayo, kampuni hiyo inaendelea na ukarabati wa jumla wa kituo hicho ili kuhakikisha abiria wanapata huduma bora, salama na za kisasa.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni, maandalizi ya kuanza ujenzi wa jengo kubwa la kupumzikia abiria pamoja na mgahawa wa kisasa yako katika hatua za mwisho na yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Hatua hizo ni sehemu ya mkakati wa Shabiby Bus kuimarisha miundombinu na kuinua viwango vya huduma katika sekta ya usafiri wa abiria, hususan katika jiji la Dodoma ambalo ni makao makuu ya shughuli za Serikali na taasisi mbalimbali za kitaifa.
Maboresho hayo yanatarajiwa kuongeza faraja, usalama na ufanisi wa huduma kwa maelfu ya abiria wanaotumia kituo hicho kila siku.



No comments:
Post a Comment