DKT. MWIGULU AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA SPENCON-MABOGINI-KAHE-CHEKERENI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 20, 2026

DKT. MWIGULU AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA SPENCON-MABOGINI-KAHE-CHEKERENI.


Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 20, 2026 amekagua ujenzi wa barabara ya Spencon-Mabogini -Kahe-Chekereni yenye urefu wa kilomita 31.25.

Akizungumza na Wananchi wa Mabogini, Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Dkt. Mwigulu ameelekeza barabara hiyo ihamishwe kutoka TARURA, na kwenda TANROADS ili ijengwe kwa kiwango cha lami kwa kuwa ni Bypass hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano katikati ya mji wa Moshi.

Nae Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa barabara hiyo inayopita katika maeneo yenye uzalishaji wa mpunga na miwa itapandishwa hadhi na kujengwa kwa kiwango cha lami kama alivvyoelekeza.

Aidha, amesisitiza kuwa barabara ya Kibosho shine- Kwarafael-International school yenye urefu wa km25.52 itajegwa haraka kwa lami km 6.4 zilizosalia,

Waziri Mkuu Dkt. Nchemba anaendelea na ziara yake ya siku nne ya kukagua miundombinu na kuzungumza na wananchi mkoani Kilimanjaro.




No comments:

Post a Comment