HUDUMA ZA BENKI YA NBC ZAKONGA NYOYO ZA WATEJA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 30, 2022

HUDUMA ZA BENKI YA NBC ZAKONGA NYOYO ZA WATEJA

Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa benki hiyo makao makuu Mussa Mwinyidaho akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo Julai 29,2022 jijini Dodoma.
Meneja wa Tawi la NBC Dodoma Happiness Kizigira akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo Julai 29,2022 jijini Dodoma.
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa benki ya NBC DK. Kassim Hussein akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo Julai 29,2022 jijini Dodoma.
Mteja wa Benki ya NBC SHEHA ABUBAKARI akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo Julai 29,2022 jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma 

Wafanyabiashara wadogo na wakati wa mkoa wa Dodoma, ambao ni wateja wa benki ya NBC wameeleza kuridhishwa na huduma zinazotolewa na benki hiyo, ikiwemo mikopo yenye riba nafuu na rafiki inayosaidia kukuza biashara zao.

Wafanyabiashara na wajasiriamali hao wakiongea wakati wa mazungumzo ya kibiashara na chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo wamesema kuwa biashara zao pamoja na taasisi zao zimekuwa zikinufaika na benki hiyo kwani kumekuwa na mikopo wakati mwingine isiyo na dhamana yeyote.

HASSAN MVUNGI ni Mfanyabiashara na pia ni mnufaika wa huduma za Benki ya NBC amesema kuwa yeye amejiunga na benki hiyo tangu mwaka 2007 na mpaka sasa ni mfanyabishara mkubwa jijini Dodoma na mtaji mkubwa wa biashara yake amepata kupitia Benki hiyo.

Naye SHEHA ABUBAKARI ambeya ni Mteja wa Benki hiyo amesema kuwa wanafurahishwa na huduma wanayoipata ambapo imesaidia katika kuinua taasisi yao hivyo anawaomba watanzania kujiunga na benki hiyo ya Taifa ya Biashara ili kunufaika katika uendeshaji wa biashara zao.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo DK. Kassim Hussein  amesema benki hiyo imerahisisha utaratibu wa upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo ya hadi kiasi cha shilingi milioni 150 bila kuwa na dhamana yoyote.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa benki hiyo makao makuu Mussa Mwinyidaho amesema mchango wa wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali katika pato la taifa ni asilimia 35, huku wakitoa ajira kati ya moja hadi 100 ambayo imeajiri takribani watu milioni 15 hapa nchini.

"Benk yetu pia  imekuja na huduma mpya ya mikopo ya nyumba ambapo mteja ukiwa na kiwanja ambacho unahitaji kujenga basi benki yetu itakupatia mkopo ukajenge alafu dhamana yetu sisi inakuwa hiyo nyumba uliyoijenga"Amesema Mwinyidaho 

Na kuongeza kuwa "Msiwe na wasiwasi hata wa kutafuta miradi mikubwa nyie tafuteni mkipata mtaleta kwetu sisi tutakusaidia kuwapatia mikopo ya kukamilisha mradi huo alafu mradi huo unakuwa dhamana yetu sisi tunataka kuwasaidia wateja wetu kupiga hatua katika biashara zao" Mwinyidaho 

Meneja wa benki hiyo ya NBC Tawi la Dodoma Happiness Kizigira amesema kuwa wateja wanahitaji huduma za kifedha na hawajua pakuzipata hivyo anwakaribisha kupata huduma hiyo kwenye benki hiyo.

"Sisi kama benki ya NBC tunachojua ni kwamba watu wanashinda sana na huduma za kifedha hivyo sisi tumedhamiria kuitatua changamoto hiyo kwa kuwapatia wateja wetu mikopo ambapo watatumia katika kuongeza mitaji katika biashara zao."Amesema Happiness 


No comments:

Post a Comment