Kamati yapita kukusanya Maoni kwa wasanii Mwanza - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 19, 2022

Kamati yapita kukusanya Maoni kwa wasanii Mwanza


SERIKALI imeunda Kamati ya kuratibu namna bora ya kusimamia hakimiliki kwa wasanii nchini ambapo inakusanya maoni toka kwa kundi hilo kwa ajili kuwasaidia kuwa na mipango ya kuboresha shughuli hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu namna Bora ya kusimamia Hakimiliki nchni Dk Saudin Mwakaje alisema leo jijini Mwanza kuwa lengo la kamati ni kukusanya maoni kutoka kwa wasanii ili kufahamu changamoto wanayokumbana ili kuziondoa.

Alisema lengo la kukusanya maoni kutoka kwa wazalishaji wa kazi za usanii yaani watunzi,waigizaji,waandishi na wazalishaji imeletwa kutokana na lengo la kutaka kuwepo kwa makusanyo makubwa kutoka kwa kundi hilo ili waweze kunufaika na kuchangia kwenye pato la taifa.

Dk Mwakaje alisema kuwa lengo la kuwa na mpango huo ni kutokana na mabadiliko ya bunge kwa sheria ya kukusanya mapato ya mwaka 2022 yanayotaka makampuni kukusanya mirahaba na kugawa kwa wasanii.

“Kupitia utaratibu huo mpya wa kutumia makampuni kukusanya mirahaba na kugawa imetulazimu tupite kwa kundi hili la wasanii ili kupata maoni yao juu ya namna bora ya kuendesha zoezi hilo” alisema Dk Mwakaje.    

Baadhi ya wasanii hao walisema kuwa umefika wakati kwa Chama cha Hatimiliki Tanzania (COSOTA) na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kufanya kazi zake kwa haraka ili kuleta mabadiliko kwenye tasnia hiyo hapa nchini ili kuwezesha kundi hilo kupata maslahi bora.
 
Mdau wa Kazi zake za Ubunifu Francis Kaswahili alizitaka COSOTA na BASATA kuangalia namna bora ya kuwezesha makundi ya wasanii kunufaika na kazi zao kwa kuweka majukumu yao sehemu ambayo itawafaya kunufaika na mchango wanaoufanya na wakati huo serikali kupata mrahaba wa kazi za usanii.
 
Msanii wa maigizo Peter Garincha alishauri kupunguzwa kwa kodi zinazotozwa kwa kundi hilo la wasanii ili kuwaondolea mzigo wa malipo mengi kwani inawahangaisha kwa sasa nchini

No comments:

Post a Comment