Idadi ya wageni 42 wametembelea Banda la NACTVET siku ya kwanza ya maonesho hayo ili kujielimisha juu ya udahili, na kupata huduma ya Namba ya uthibitisho wa tuzo (AVN) na wengine kujua namna ya kuanzisha vyuo vya kutoa ujuzi kwa muda mfupi kwa mfumo wa vituo vya mafunzo ya ufundi stadi.
Maonesho hayo ambayo Kauli mbiu yake ni: Elimu ya Juu Inayokidhi Mahitaji ya Soko la Ajira kwa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi yamefunguliwa rasmi leo tarehe 19/7/2022 na waziri mkuu Kassim Majaliwa.
NACTVET inakukaribisha kupata huduma !
No comments:
Post a Comment