KUELEKEA SHEREHE YA EID EL HAJ, SHEIKH MKUU WA MKOA WA DODOMA ATAJA WANYAMA WANAORUHUSIWA KUCHINJWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 9, 2022

KUELEKEA SHEREHE YA EID EL HAJ, SHEIKH MKUU WA MKOA WA DODOMA ATAJA WANYAMA WANAORUHUSIWA KUCHINJWA


Na Mwandishi wetu DODOMA

SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu amewataja wanyama ambao wanaruhusiwa kuchinjwa katika sherehe ya Eid el Haj kuwa ni wale wote wenye miguu minne, wanaoliwa na kufugwa na binadamu.

Akizungumza na wandishi wa habari Jana jijini hapa Sheikh Rajabu aliwataja wanyama hao kuwa ni mbuzi, kondoo, ngamia na ng'ombe.

"Sikukuu ya Eid el Haj ni siku maalumu kwa ajili ya kuchinja wanyama ambapo historia yake inaanzia kwa Ibrahim pale alipooteshwa ndoto kwamba amchinje mwanaye Ismaili, hivyo hakukurupuka bali alimwadisia mwanaye ndoto hiyo ndipo Ismaili akamwambia Baba fanya utakalo na mimi utanikuta mwenye amani,"

Aliongeza kuwa "Wakati Ibrahim anachukua kisu chake kutaka kumchinja mwanaye ndipo Mwenyezi Mungu akamtuma Malaika Jibril akiwa na mnyama kondoo akamwambia umefaulu mitihani sasa muache mwanao na umchinje huyu kondoo.

Sheikh Rajabu alisema tukio hilo la Ibrahimu ndio linapelekea kutokea sikukuu ya Eid el Hajj maana yake ni Eid ya kuchinja.

Alisema kwa watu wenye uwezo wanatakiwa kuchinja wanyama wenye miguu minne na wanaoliwa na kufugwa na binadamu wakiwemo Kondoo,ngamia,mbuzi na ng'ombe.

"Hata hao wanyama wanaochinjwa wanatakiwa wasiwe na aibu yaani hawakuvunjwa pembe, hawakukatwa masikio, na wasiwe vilema, wanyama hao wanatakiwa kuchinjwa baada ya kutoka katika ibada ya suna ya swala ya Eid shughuli za uchinjaji ziendelee,"alisema

Katika hatua nyingine Sheikh Rajabu alisisitiza jamii kumrudia Mwenyezi Mungu na kuachana na matendo yote ambayo hayampendezi ikiwemo masuala ya ukatili,wizi, na unyanyasaji wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment