MAHUBIRI NDANI YA MABASI MARUFUKU-LATRA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 26, 2022

MAHUBIRI NDANI YA MABASI MARUFUKU-LATRA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo akizungumza na waandishi wa habari akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Julai 26,2022 Jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya mabasi kuruhusu biashara,Mahubiri mbalimbali ya dini na video zisizofaa kwa sababu ni kinyume na kanuni za usafirishajii.

Amepiga marufuku hiyo jijini Dodoma julai 26,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na kubainisha kuwa mamlaka hiyo ina jukumu kubwa la kudhibiti ubora ,viwango na usalama wa huduma.

Amesema kuwa biashara na kutoa mahubiri imeshakuwa tabia kwa baadhi ya vyombo vya Usafirishaji hapa nchini jambo ambalo limekuwa kero kwa wasafiri hivyo ni vyema wamiliki pamoja na watoa huduma kuachana kabisa na tabia hizo kwa sababu ni ukiukwaji wa kanuni zinazoongoza sekta hiyo.

"Kwanzia leo napiga marufuka biashara zote zinazofanyika kwenye vyombo vya usafiri na Mahubiri ni marufuku kufanya hivyo ni kinyume na sheria hivyo tabia hizo zikome ni kero kwa wasafiri"Amesema Suluo

Kwa upande mwingine CPA Suluo amesema kuwa mpaka sasa kupitia mamlaka hiyo imeshafunga mfumo wa VTC kwa mabasi 7502 na hayo ndio mabasi yanayoruhusiwa kufanya biashara ya usafishaji wa habiria hapa nchini.

Na kuhusu Madereva waliosajiliwa na kupewa leseni kwa ajili ya magari ya usafirishaji idadi yake ni 10324 hivyo kuwataka wamiliki kuhakikisha wanawaajiri madereva wenye sifa stahiki.

Pamoja na hayo CPA Suluo amepiga marufuku pia kwa mabasi yanayokatisha ruti,Mwendokasi na baadhi ya mabasi ambazo wahudumu wake wanatuhumiwa kunyanyasa abiria hususani watoto wa shule.

"Kiukweli kuna baadhi ya mabasi yana tabia ya kukatisha ruti bila sababu,wengine wanaendesha magari mwendokasi bila sababu na kuwanyanyasa abiria hususani hawa watoto wa shule alafu unakuta kuna baadhi ya wazazi wapo hapo na wanashuhudia kabisa mtoto ananyanyaswa na wanatulia tu tujitahidi kuwa na uchungu maana hawa wanafunzi ni taifa la kesho"Amesisitiza CPA Suluo

Naye Mkurugenzi wa uthibiti usafiri barabarani LATRA ,Johansen Kahatano ameeleza kuwa Kwa mabasi yanayokwama njiani sheria inaelekeza ndani ya saa mbili abiria anaruhusiwa kuendelea na safari kwa gharama zake mwenyewe na baada ya siku saba adai haki yake aliyotumia.

Pia ameeleza kuwa iwapo abiria atakuwa ameridhia kusubiri ili aweze kuendelea na safari mmiliki au kampuni inatakiwa kutoa huduma zote za kibinadanu kwa maana ya kula, kunywa na kulala.

No comments:

Post a Comment