TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WASHIRIKA WA MAENDELEO NA WADAU BINAFSI ILI KUKUZA TEKNOLOJIA NCHINI-YONAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 26, 2022

TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WASHIRIKA WA MAENDELEO NA WADAU BINAFSI ILI KUKUZA TEKNOLOJIA NCHINI-YONAZI

Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jimmy Yonazi akizungumza wakati wa Kikao cha kusaini MOU ya Kongamano la C2C na Kampuni ya Extensia Limited kutoka nchini Uingereza hafla iliyofanyika Julia 25,2022 jijini Dodoma kushoto ni mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya hiyo Tariq Malik
Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jimmy Yonazi akitia saini MOU ya Kongamano la C2C na Kampuni ya Extensia Limited kutoka nchini Uingereza hafla iliyofanyika Julia 25,2022 jijini Dodoma kushoto ni mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya hiyo Tariq Malik
Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jimmy (Kulia) na Kushoto ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Extensia Limited Tariq Malik wakionesha mikataba hiyo baada ya kutia saini Julia 25,2022 jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma 

Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jimmy Yonazi amesema kuwa wataendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo na wadau binafsi ili kuhakikisha kwamba wanakabiliana na maendeleo ya sasa ya teknolojia.

Ameyasema hayo Julia 25,2022 jijini Dodoma wakati wa Kikao cha kusaini MOU ya Kongamano la C2C na Kampuni ya Extensia Limited kutoka nchini Uingereza ambapo amesema kuwa Madhumuni ya mkutano huo wa C2C ni kuboresha muunganisho na miundombinu na kushughulikia masuala yanayohusiana na kuongeza kasi ya uwekezaji na utekelezaji wa miundombinu ya kidijitali.

Yonazi ameongeza kuwa Mkutano wa C2C 2022 umebuniwa na Extensia ili kusaidia nchi zinazotaka kuharakisha mabadiliko yao ya kidijitali kwa kutumia teknolojia na uwekaji miundombinu, kuunganisha watumiaji wa mwisho, watoa huduma na watunga sera na wawekezaji, wachuuzi na watoa suluhisho katika mazingira mahususi ya biashara.

Aidha kuelekea Kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika kwa siku mbili mwezi Septemba 2022 Yonazi amebainisha kuwa makubaliano walioingia kati ya wizara hiyo na Extensia yamefafanua kwa uwazi wajibu wa kila pande ili kuhakikisha kuwa mkutano wa C2C 2022 unatekelezwa kwa mafanikio.

"Kwa dunia hii ya sasa ya Uchumi wa kidijitali na mapinduzi ya nne ya viwanda, hutegemea sana matumizi ya TEHAMA hivyo lazima tuhakikishe eneo hili tunaliboresha kisawa sawa" Amesema Jimmy Yonazi

Mkutano wa C2C uliratibiwa na Extensia Limited nchini Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo mwaka 2013, 2014 na 2015 kwa ushirikiano na Wizara,NICTBB,TTCL,TCRA ili kusaidia mradi wa Taifa wa TEHAMA kuwa wa kibiashara kwa nchi jirani na mataifa mengine ya Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema kuwa mkutano huo utakuja na matokeo mazuri ya muelekeo wa ukuaji wa TEHAMA hapa nchini ikiwemo utatuzi wa changamoto za kimtandao kwani utahusisha watu kutoka maeneo mbalimbali Duniani ambao watakuja na mawazo yao na bunifu.

Aidha,Mulembwa amebainisha kuwa ifikapo mwaka 2023 wanatarajia kukamilisha kuinganisha nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenye Mkongo wa Mawasiliano ya Taifa ikiwa ni nchi ya nane kwa ukanda huu wa Afrika ya mashariki na kati na nchi zilizoizunguka Tanzania.

"Tunataka Tanzania iwe kitovu cha mawasiliano mpaka sasa tumeshaunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika nchi saba zinazotuzunguka ambapo tumebakiza nchi moja tu ambayo ni Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) nayo mpaka ifikapo mwaka 2023 tutakuwa tumeshaunganisha",Amesema Mulembwa

Na kumalizia kuwa "Kongamano hili Litaleta makampuni makubwa sana ya mwasiliano Duniani ambayo itatupatia uzoefu lakini nao pia watapata nafasi ya kujifunza kutoka kwetu hivyo ni kongamano muhimu sana naamini baada ya hapo tutapiga hatua zaidi katika mawasiliano",Mulembwa

No comments:

Post a Comment