Maonesho hayo yameshirikisha wadau mbalimbali wa kilimo kutoka sekta binafsi na serikali ambapo Mavunde alipata wasaha wa kutembelea mashamba ya mfano yanayotumiwa na TARI kufundishia kilimo na kufanyia utafiti; Mashamba hayo ni ya mahindi, ngano na mazao ya mboga mboga.
Amepata kujua namna ambavyo teknolojia inatumiwa kuongeza thamani ya mazao kisha akaenda kukagua mabanda ya wadau mbalimbai wa kilimo waliokuwa wakionesha bidhaa za kilimo.
Katika hotuba yake Mavunde amewataka wakulima nchini na wadau wote wa kilimo kufanya kilimo kuwa cha kibiashara hasa kwa kutumia teknolojia katika kuongeza thamani katika mazao.
Amesema uamuzi huo utaongeza kiwango cha uuzaji wa mazao kwenda nje ya nchi na kuwa serikali itaendelea kushirikana na wadau mbalimbali katika kutafuta masoko kimataifa.
Mavunde amebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inauza parachichi nchi za India, Afrika Kusini, Hispania na kuna mazungumzo ya kuuza parachichi kwenda China na Marekani.
#Ajenda1030 #KilimoNiBiashara




No comments:
Post a Comment