MHE. SIMBACHAWENE APONGEZA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI ANWANI ZA MAKAZI KIBWAKWE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 11, 2022

MHE. SIMBACHAWENE APONGEZA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI ANWANI ZA MAKAZI KIBWAKWE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene akizungumza na wananchi wa kata ya Pwaga na Luhundwa alipotembelea na kufanya mikutano ya hadhara katika jimbo la kibwakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

Na mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kutekeleza vizuri zoezi la anwani za makazi.

“Uwekaji wa anwani za makazi unaenda sambamba na zoezi la sensa ili kujua katika ramani mahali mitaa, barabara zilipo. Mmefanya jambo zuri ambalo watu wengine wanapaswa kuja kujifunza alisema waziri”

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe George Simbachawene katika ziara aliyoifanya Kata ya Pwaga na na Luhundwa alipotembelea na kufanya Mikutano.

“Haya ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza operesheni ya postikodi ili watanzania wajulikane wanakaa wapi; jambo la kuweka mitaa, lakini pia barabara na namba kwenye nyumba katika Halmashauri wilaya ya Mpwapwa na jimbo la Kibakwe limefanyika kwa mazingira makubwa”

No comments:

Post a Comment