Na mwandishi wetu Dar-es-salaam
Mratibu Mwandamizi kutoka NACTVET, bi.Levina Lunyungu (pichani) anaendelea kutoa huduma kwa wageni wanaohitaji namba ya uthibitisho wa tuzo (AVN) ikiwa ni moja kati ya huduma nyingi zinazotolewa katika Banda hilo
Wakati huohuo Wanafunzi wengi waliomaliza masomo ya stashahada wanaotaka kuendelea na masomo ya shahada nao wanatembelea Banda la NACTVET kupata huduma hiyo.
Aidha, wananchi wengi wanaotembelea Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 28 Juni 2022 wanapata maelezo mbalimbali kuhusu majukumu ya Baraza na huduma zingine ikiwemo namna ya kuanzisha chuo cha ufundi cha kati na vile vile wanapatiwa mwongozo kuhusu hatua za kuanzisha Chuo cha ufundi stadi (VTC).




No comments:
Post a Comment