Na Okuly Julius-Dodoma
Mtakwimu mkuu wa serikali DK. ALBINA CHUWA, amesema maandalizi ya sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022, itakayofanyika Agosti 23 yamefikia asilimia 87 hadi sasa, huku asilimia 97 ya wananchi ambao wamehojiwa juu ya kufanyika kwa zoezi hilo wakionyesha utayari wa kushiriki kwenye sensa hiyo.
Akizungumzia kuanza kwa mafunzo ya wakufunzi wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, iliyoanza leo Julai 6 katika ngazi ya mkoa kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, Dk. CHUWA, amesema mwamko wa sensa ya mwaka huu ni mkubwa kutokana na uhamasishaji unaoongozwa na Rais Samia Suluhu
Aidha, mtakwimu mkuu huyo wa serikali amewahakikishia wananchi usalama wa taarifa zao watakazozitoa kwa wasimamizi na makarani wa sensa.
"Nawahakikishia wananchi usalama wa taarifa zao kuweni huru kwa sababu hiyo ni siri baina yako wewe na Karani na kuna adhabu zimewekwa kwa mujibu wa sheria zitakazotumika kwayeyote yule atakayevujisha hizo taarifa,"Amesema Dk.CHUWA
Kwa mujibu wa Dk. ALBINA CHUWA, washiriki wa mafunzo ya sensa katika ngazi ya mkoa yatakayofanyika kwa siku 21 kuanzia Julai 6 hadi Julai 26 mwaka huu ni waratibu wa sensa wa wilaya, maafisa elimu mkoa na wilaya, wataalam wa TEHAMA wa wilaya, maafisa maendeleo ya jamii wa wilaya, maafisa mipango wa wilaya, waratibu elimu kata pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya watu wenye ulemavu nchini.
Kwa taarifa zaidi video ifuatayo inafafanua zaidi juu ya ulinzi na usalama wa taarifa zote za wananchi zitakazochukuliwa siku hiyo ya Sensa kitaifa Agosti 23,2022 na ikibainisha pia adhabu zitakazochukuliwa kwa makarani watakaovujisha taarifa.
No comments:
Post a Comment