![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea siku ya Mashujaa kitaifa mara baada ya kutembelea viwanja vya mashujaa jijini Dodoma kujionea maandalizi hayo. |
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Dodoma akiwa ameambatana na katibu tawala mkoa upande wa kushoto Dkt.Fatuma Mganga wakikagua maandalizi ya sherehe za mashujaa kwenye mnara wa mashujaa jijini Dodoma. |
![]() |
Mkurugenzi wa maadhimisho kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Batholomeo Jungu akielezea jinsi maandalizi yanavyoendelea kuelekea siku ya mashujaa kitaifa. |
![]() |
Baadhi ya mafundi wakiendelea kukarabati mnara wa mashujaa jijini Dodoma kuelekea siku ya kitaifa ya mashujaa. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika sherehe ya siku ya mashujaa kitaifa yatakayofanyika Julai 25,2022 katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma.
Akikagua maandalizi kuelekea siku hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema maandalizi ya sherehe hizo yanakwenda vizuri na yeye kama mwenyeji ni vyema kufika kujionea mwenendo wa maandalizi hayo.
"Mimi kama mwenyeji wa sherehe hizi ni vyema kufika kujionea mwenendo wa maandalizi haya hii ni siku muhimu pia kwa taifa kwa sababu tutakuwa tunakumbuka mashujaa wetu waliopambana kwa ajili ya taifa letu na kutupatia uhuru na amani ambayo mpaka sasa tunajivunia hivyo ni siku muhimu sana na tunatarajia ugeni mkubwa ukiongozwa na Mhe.Rais Samia ambae ndiye atakuwa mgeni rasmi"Amesema Mtaka
Aidha,Mtaka amesema kuwa usiku wa Julai 24 ,2022 utawashwa mwenge kuamkia siku ya mashujaa kitaifa Julai 25,2022.
Mtaka pia amewataka wananchi wa mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa ya kuweka huduma mbalimbali kwenye viwanja hivyo ikiwemo huduma ya Chakula na wale wenye vivutio vya kitalii watumie fursa hiyo kujitangaza.
"Niwakaribishe wanadodoma kuweka biashara zao hapa kwenye viwanja hivi ikiwemo chakula na bidhaa zingine za kitalii hiyo pia itawasaidia kuongeza kipato " Amesema Mtaka
Awali mkurugenzi wa maadhimisho kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Batholomeo Jungu amesema maandalizi ya maonesho hayo yanaendelea vizuri.
Siku ya Maadhimisho ya Mashujaa hufanyika Julai 25 kila mwaka kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa wa taifa waliopoteza maisha kwa kulipigania taifa lao na kulinda uhuru na hufanyika shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalum na gwaride maalum ambapo mwaka huu kitaifa yakifanyika jijini Dodoma na mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment