Tume ya Madini imefanikiwa kupata hati safi kwa mara nyingine kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020-2021 kutokana na usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha katika shughuli zake.
Hayo yamesemwa na wakaguzi wa nje kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali katika kikao na menejimenti ya Tume jijini Dodoma ambapo sambamba na kupongeza Tume ya Madini kufanya vizuri kwenye usimamizi wa matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali wameitaka Tume ya Madini kuendelea kuboresha huduma zake kwa wadau wa madini.
No comments:
Post a Comment