KANISA LA EAGT DODOMA LAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, August 7, 2022

KANISA LA EAGT DODOMA LAMPONGEZA MHE.RAIS SAMIA

Askofu Mkuu wa Kanisa EAGT Dodoma Dkt.Brown Abel Mwakipesile akihubiri neno la Mungu katika ibada ya leo Agosti 7,2022 iliyofanyika katika kanisa hilo
Baadhi ya Waumini wa Kanisa la EAGT Dodoma wakifutilia mahubiri yanayotolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt.Brown Abel Mwakipesile wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisa hilo leo Agosti 7,2022 jijini Dodoma.

NA Winner Marawiti-Dodoma

Kanisa la EAGT Dodoma limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluh Hassan kwa maendeleo anayoyafanya katika nyanja mbalimbali ikiwepo kuitangaza nchi  kimataifa.

Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt.Brown Abel Mwakipesile wakati akizungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa wanaiombea serikali ya Rais Samia pamoja na uongozi wake kwa jitihada kubwa zinazofanywa ili kulipeleka taifa mbele.

Aidha ,Askofu Dkt. Mwakipesile ametoa shukrani pamoja na pongezi kwa serikalii kwa namna inavyotoa nafasi na vibali katika kueneza Neno la Mungu.

''Naishukuru sana Nchi yetu kwa vile ambavyo imetoa uhuru wa kwamba neno la Mungu lihubiriwe kwa watu wote katika Nchi yetu kwa sababu neno la Mungu ndio Baraka na Ufunguo pekee katika Maisha ya Mwanadamu''Askofu Mwakipesile.

Hata hivyo Askofu Mwakipesile amebainisha kuwa katika mkutano uliokuwa ukifanyika kanisani hapo ambao utahitimishwa leo umekuwa mkutano wa baraka na muujiza mkubwa ambapo watu wengi wamefunguliwa vifungo vilivyokuwa vinatesa maisha yao.

No comments:

Post a Comment