Na Mwandishi wetu - Mbeya
Akizungumza baada ya kuzindua Miundombinu iliyojengwa na kukarabatiwa na Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Canda kupitia Mradi wa Kuboresha Vyuo vya Ualimu Nchini, amesema ukarabati huo utakwenda sambamba na uboreshaji wa mitaala pamoja na mapitio ya Sera ya Elimu ya Mwaka 2014.
"Ninaipongeza Wizara ya Elimu kwa kusimamia vyema mradi huu, na ninashukuru Serikali ya Canada kwa kufadhili mradi huu, Waziri wa elimu amenieleza mnakamilisha mazungumzo ili kutoa ufadhili wa awamu ya pili. Natumai mazungumzo yatakwenda vizuri na awamu ya pili kuanza,"amesema Mhe. Samia
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema ukarabati na uboreshaji wa Miundombinu katika Vyuo vya Ualimu ni sehemu ya mikakati ya Wizara ya kuleta mageuzi katika Sekta kwa kuhakikisha elimu inatoa ujuzi ili kuandaa wahitimu wanaoendana na soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Prof. Mkenda ameongeza kuwa Wizara inakamilisha Rasimu za Sera na Mitaala ya Elimu Msingi na kwamba Wizara itakuwa na kongamano kubwa litakalofanyika Mwezi wa Kumi la kupokea maoni kutoka kwa wadau juu ya rasimu ya Mitaala na ya Marekebisho ya Sera ya Mwaka 2014.
Mradi wa UTC unaosimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia umefanya ujenzi na ukarabati katika Vyuo vya Ualimu vinne ambavyo ni Chuo cha Ualimu Mpuguso, Ndala, Kitangali na Chuo cha Ualimu cha Shinyanga na umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 39.7 ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania na Canada.
No comments:
Post a Comment