SHILINGI BILIONI 9.9 KUTUMIKA KWA AJILI YA KUJENGA MAABARA KATIKA MIKOA YA KIMKAKATI-TBS - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 1, 2022

SHILINGI BILIONI 9.9 KUTUMIKA KWA AJILI YA KUJENGA MAABARA KATIKA MIKOA YA KIMKAKATI-TBS

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Dkt.Athuman Ngenya akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma kuhusiana na utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2022/2023
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Dkt.Athuman Ngenya leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma wakati akizungumzia utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwa shirika hilo.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo GERSON MSIGWA akizungumza mara baada ya wasilisho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Dkt.Athuman Ngenya mbele ya waandishi wa habari leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwa shirika hilo.

Na Okuly Julius-Dodoma

Serikali imetenga kiasi cha TZS 9.9 Billioni kwa ajili ya kujenga jengo la maabara (Viwango House) katika miji ya kimkakati (Dodoma na Mwanza) ili kusogeza huduma za Shirika la viwango Tanznania (TBS) karibu kwa wateja na kuongeza ufanisi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Athuman Ngenya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma kuhusiana na utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2022/2023 ambapo amesema kuwa kwa sasa Maabara ipo Moja tu ya Dar-es-salaam makao mkuu jambo ambalo linasababisha kucheleweshwa kwa huduma.

Dkt.Ngenya amesema kuwa katika kuhakikisha usalama wa vyakula na vipodozi kwa taifa unakuwpo shirika limeona ni vyema kujenga maabara hizo ili kuondasha ile adha iliyopo kwa sasa ya kusafiri kutoka mbali kupeleka bidhaa maabara kuu ya Dar-es-salaam kupima ubora na itasaidia pia kuharakisha maendeleo ya watoa huduma.

"Unakuta mtu anatengeneza mkate wake huko Kagera sasa ili kupitishwa kwa ajili ya kuingizwa sokoni kwa maana ya kuanza kutumika na wananchi ni lazima asafirishe mpaka Dar-es-salaam kwa ajili ya kupimwa ubora sasa embu fikiria kutoka Kagera mpaka Dar-es-salaam hapa katikati inaweza ikatokea chochote ikaoza ama ikapata changamoto sasa unakuwa umepoteza muda"Amesema Dkt.Ngenya

Pia Dkt.Ngenya amesema Shirika limetenga kiasi cha TZS 2.7 Billioni kwa ajili ya kuimarisha ofisi saba za kanda za shirika katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam, Dodoma, Kigoma na Mbeya.

Fedha hizo pia zitatumika kuimarisha ofisi za shirika hilo mipakani ikiwemo Tunduma, Kasumulo, Horohoro, Holili, Tarakea, Namanga, Bandari ya Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro,Sirari, Kabanga, Rusumo, Mtukula, Bandari ya bagamoyo, bandari ya Dar es salaam, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere- Dar, Bandari ya Tanga)

"Pia tutaongeza wafanyakazi na vitendea kazi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakati na kuimarisha zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara sokoni ili kupunguza bidhaa hafifu sokoni na hatimaye kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora na salama" amesema Dkt.Ngenya

Amesema pia shirika hilo limetenga TZS 1.6 Billioni kwa ajili ya kuandaa viwango 630 vya kitaifa katika sekta mbalimbali ili kuwezesha biashara kwa kumpa uhakika mzalishaji wa kupata masoko ya ndani na nje, kumhakikishia mlaji wa mwisho usalama na ubora wa bidhaa atakayotumia ikiwa ni pamoja na kuweka ushindani sawia wa bidhaa katika soko.

Dkt.Ngenya ameongeza kuwa ili kuhakikisha wananchi wanatumia bidhaa zilizo bora na salama Shirika hilo pia limetenga TZS 261 Millioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za usajili wa bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi.

Pamoja na hayo Dkt.Ngenya amebainisha kuwa Shirika hilo pia limetenga TZS 581 Millioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uthibitishaji wa mifumo ya kiutendaji ambapo kwa sasa TBS imepatiwa ithibati ya kufanya shughuli hiyo na mashirika yanaweza kuthibitishiwa ubora wa mifumo yao ya kiutendaji kupitia hii itasaidia kuhakikisha wananchi wanapokea huduma zilizo bora.

Amesema Katika kufanya shughuli za kuhakiki ubora wa vipimo ili kuhakikisha usahihi wa majibu ya vipimo mbalimbali kutokea maabara, mahospitalini na viwandani na kupelekea watoa huduma au maamuzi kufanya maamuzi sahihi Shirika hilo limetenga TZS 800 Millioni.

Shirika limetenga TZS 1.18 Billioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ukaguzi wa bidhaa kabla ya kusafirishwa kuja nchini (PVoC) na baada ya kuwasili nchini (Destination Inspection) ili kuhakikisha nchi haiwi jalala la kupokea bidhaa zilizopigwa marufuku au hafifu.

Shirika la viwango Tanznania (TBS) linaendelea na juhudi za kuweka na kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuboresha huduma zake kwa lengo la kuwezesha biashara kwa dhumuni la kuinua uchumi wa viwanda kwa kuchagiza uzalishaji wa bidhaa salama na bora hapa nchini kama njia mojawapo ya kuchangia pato la Taifa letu.


No comments:

Post a Comment