TUNATENGENEZA AJIRA KWA MADEREVA 1,600 KILA SIKU - TPA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, August 13, 2022

TUNATENGENEZA AJIRA KWA MADEREVA 1,600 KILA SIKU - TPA

Mkurugenzi wa Mipango,Ubora na udhibiti vihatarishi wa Mamlaka hiyo Dkt.Boniphace Nobeji wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022-2023.

Na Okuly Julius-Dodoma

Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebainisha kuwa wanatengeneza wastani wa ajira za madereva 1,600 kila siku kutokana na magari yanayo shushwa na kutolewa nje ya Bandari ya Dar es saalaam ambapo ni wastani wa magari 600 na wastani wa magari ya kubeba Mizigo 1,000 huingia kupakia na kushusha shehena Bandarini hapo.

Mamlaka hiyo imesema kuwa kuna kampuni za Mawakala wa Forodha zaidi ya 500 zinazo fanyakazi Bandarini nazo zimetoa ajira kwa watanzania na jitihidi za kuendelea kupunguza idadi kubwa ya vijana ambao hawajapata ajira hapa nchini zinaendelea kwa kuboresha na kuongeza idadi ya bandari hasa katika maziwa ikiwemo Victoria, Tanganyika na katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mipango,Ubora na udhibiti vihatarishi wa Mamlaka hiyo Dkt.Boniphace Nobeji wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022-2023.

Dkt.Boniphace Amesema kuwa Sekta ya Bandari imetengeneza ajira zisizo za moja kwa moja ambazo wananchi hujipatia vipato kwa kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaofanya kazi katika sekta ya Bandari kama vile,Kuuza vipuli vya mitambo ya magari yanayo fanya kazi Bandarini, huduma za kifedha, kuchapisha nyaraka, chakula, vinywa.

Aidha Dkt.Boniphace amesema kuwa matarajio ya serikali ni kuhakikisha biashara zinaimarishwa na wao kama Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania wanafanya hivyo ili kuendana na kasi ya maendeleo ya taifa.

"Sisi tupo vizuri katika kuhakikisha matarajio makubwa ya serikali iliyonayo kupitia Mamlaka yetu hivyo tunahakikisha ajira zinazalishwa za kutosha ,lakini pia mapato yanapatikana na hilo ndio la msingi"Amesema Dkt.Boniphace

Na kuongeza kuwa " kazi kubwa inayofanywa na serikali ni lazima sisi kama mamlaka zake tuunge mkono hizo juhudi na sisi kama mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania tumejipambanua katika eneo hilo ndio maana katika ajira tunatengeneza zaidi ya ajira 1600 sio kazi ndogo hiyo ndugu zangu wanahabari,"Ameongeza Dkt.Boniphace

Kwa upande wa Mchango Katika Kuhakikisha Usalama wa Nchi Dkt.Boniphace amesema kuwa Mamlaka hiyo Ili kuhakikisha kwamba Sekta ya Bandari inachangia katika ukuaji wa uchumi na pato la Taifa.

"Maeneo ya Bandari yanatakiwa kuwa na usalama unaokidhi viwango vya kimataifa hali hii huwajengea imani watumiaji wa Bandari kuwa Shehena na Mali zao zingine ziko salama chini ya usimamizi wa Bandari" Dkt.Boniphace

Na kuongeza "Ili kudumisha hali ya ulinzi na usalama katika Bandari na maeneo yanayozunguka Bandari, TPA inashirikiana na vyombo vyote vya dola kuhakikisha Bandari zote ziko salaama"Amesisitiza Dkt.Boniphace

Aidha, Dkt.Boniphace ameongeza kuwa TPA imejipanga kuhakikisha kuna udhibiti wa hali ya juu wa usalama wa Mazingira kwa kutekeleza sheria na miongozo mbalimbali ya nchi na ile inayotolewa na IMO kwa lengo la kudhibiti uchafuzi wa mazingira.

Katika Mchango wa Makusanyo ya Mapato ya Nchi Dkt.Boniphace amesema kuwa Bandari ni lango kuu la Biashara Kimataifa kati ya nchi ya Tanzania na nchi mbalimbali zinazo hudumiwa na Bandari za Tanzania.

"Bandari ya Dar es salaam inahudumia zaidi ya asilimia 95 ya Shehena zote zinazo pitia katika Bandari za Tanzania kwenda nchi jirani na hivyo kuchangia kiasi kikubwa katika makusanyo ya Kodi na Mapato mengine yasiyo ya kodi (kupitia Tozo) kwa Taifa,"Amesema Dkt.Boniphace

Dkt.Boniphace ameongeza kuwa bandari ya Dar es salaam kuna Taasisi Zaidi ya 30 za umma zinazotoa huduma mbalimbali ndani ya Bandari, mbali na wadau wengine toka Taasisi binafsi na huduma hizi hulipiwa tozo na hivyo huwa ni vyanzo vya mapato kwa Taasisi zenyewe na Taifa kwa ujumla.

" Kwa mfano Mapato yaliyo kusanywa na TPA tu kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Juni, 2022) yamefikia shilingi TZS 1.09 Trilioni na kulingana na taarifa mbalimbali za kiuchumi ni kati ya asilimia 38- 40 ya mapato yote yanayo kusanywa na TRA huchangiwa na Mamlaka yetu ya Bandari "Amemalizia Dkt.Boniphace

No comments:

Post a Comment