![]() |
Katibu wa Chama cha Himofilia Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Utengamao Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Abdalla Makala akizungumza wakati wa mafunzo hayo. |
![]() |
Dkt. Angela Forsyth ambaye ni Mfiziotherapia kutoka Marekani akionyesha kwa vitendo namna ya kumuhudumia Mtoto anaeugua Ugonjwa wa Himofilia. |
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Jengo la Watoto, Hospitali ya Taifa Muhimbili yaliratibiwa na Chama cha Himofilia Tanzania (Tanzania Haemophilia Association) kwa kushirikiana na Taasisi ya Save One life ya nchini Marekani yalilenga kuwajengea uwezo wataalamu hao kuhusu namna ya kuwahudumia wagonjwa wa Himofilia.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Katibu wa Chama cha Himofilia Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Utengamao Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Abdalla Makala alisema kuwa Wafiziotherapia na Wauguzi wengi nchini hawana uelewa kuhusu ugonjwa wa Himofilia na namna ya kumuhudumia mgonjwa mwenye tatizo hilo jambo linaloweza kupelekea madhara kwa wagonjwa ikiwemo kupata ulemavu wa kudumu.
"Kwa Mfiziotherapia ambaye hana uelewa kuhusu Himofilia akipata mgonjwa ambaye damu imevuja kwenye maungio (Joints) au misuli akimuhudumia mgonjwa huyu kama wagonjwa wengine anaweza kumsababishia changamoto zaidi ikiwemo kusababisha uvimbe zaidi au ulemavu", alisema Bw. Makala
Amesema wauguzi watapatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuwachoma sindano wangonjwa hao, lakini wagonjwa pia watafundishwa namna ya kujichoma sindano wenyewe wakiwa nyumbani.
Kwa upande wake Mtaalamu kutoka Taasisi ya Save One life. Dkt. Angela Forsyth ambaye ni Mfizotherapia kutoka Marekani amesema kuwa taasisi yao inasaidia vyama vya Himofilia kwa kuwajengea uwezo, pia inasaidia wagonjwa kwa kuwapa msaada wa dawa, mitaji midogo midogo pamoja na kufadhili masomo kwa watoto wenye tatizo la Himofilia.
Nae Bw. Alex Fransics .kutoka Mtwara ambaye ni mshiriki wa mafunzo amekishukuru Chama cha Himofilia Tanzania kwa mafunzo hayo ambayo yataleta chachu na kuchangia uelewa katika utoaji huduma kwa kuwa tatizo la Himofilia ni jipya hata kwa baadhi ya watoa huduma za afya.
Himofilia ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wa kuganda ambao unasababishwa na ukosefu wa chembe za Protini zinazosaidia damu kuganda, hivyo hupelekea mgonjwa kutoka damu muda mrefu pindi anapopata jeraha
No comments:
Post a Comment