KATIBU MKUU AWAHIMIZA WATAALAM KUONGEZA KASI UJENZI MJI WA SERIKALI DODOMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 13, 2022

KATIBU MKUU AWAHIMIZA WATAALAM KUONGEZA KASI UJENZI MJI WA SERIKALI DODOMA.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akizungumza wakati wa kikao na Timu ya Wataalam wa Kuratibu Ujenzi wa Mji wa Serikali na Taasisi za uendelezaji wa Miundo Mbinu Jijini Dodoma kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo .
Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Bwa. Meshach Bandawe (kushoto) akitoa ripoti ya Ujenzi wa Mji wa Serikali Jijini Dodoma wakati wa Kikao hicho.
Timu ya Wataalam wa Kuratibu Ujenzi wa Mji wa Serikali na Taasisi za uendelezaji wa Miundo Mbinu Jijini Dodoma wakati wa kikao hicho.

(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Dkt.John Jingu ameongoza kikao cha Timu ya Wataalam wa Kuratibu Ujenzi wa Mji wa Serikali Jijini Dodoma ,kikao hicho kimehusisha wataalam na Taasisi za Uendelezaji wa Miundo Mbinu.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Katibu Mkuu John Jingu amesema utaratibu wa Manunuzi Ukamilike Mapema kwa kuzingatia ubora  ili kuwezesha Mradi kukamilika kwa haraka.

No comments:

Post a Comment