POSTA YASHIRIKI KONGAMANO LA AfCFTA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 12, 2022

POSTA YASHIRIKI KONGAMANO LA AfCFTA

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo (kushoto) akiambatana na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika Bw. Constantine Kasese (kulia) wakati wakiwasili katika Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akisalimiana na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo mara baada ya Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Amour Hamil Bakari (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo mara baada ya Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Posta wanaotoa huduma katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Aliyeketi kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika Bw. Constantine Kasese

📍JNICC -Dar es Salaam 📍

Shirika la Posta Tanzania linashiriki kwenye Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo umefanywa leo tarehe 12 Septemba, 2022 na *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.* 

Kongamano hilo ni la siku tatu na lina lengo la kuwawezesha wanawake na vijana kufanya biashara zao kwa uhuru huku wakinufaika na soko lililopo.

Aidha, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo amehudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo lililoambatana na maonesho ya biashara na huduma mbalimbali limehudhuriwa na viongozi kutoka ndani na nje ya nchi, huku Posta ikishiriki kama mdau wa biashara nchini na Afrika kwa ujumla.

Shirika la Posta lipo ukumbini hapo kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma huduma za Sanduku la kieletroniki (kupitia Posta Kiganjani), Duka Mtandao la Posta pamoja na huduma ya kutuma mizigo, barua,vipeto na vifurushi.

Katika ufunguzi huo, Bw. Macrice Mbodo aliambatana na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika Bw. Constantine Kasese.

*Imetolewa na:*
*Kitengo cha Mawasiliano,*
*Shirika la Posta Tanzania,*
*12 Septemba ,2022*

No comments:

Post a Comment