![]() |
WAZIRI Wa Afya Ummy Mwalimu,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Septemba 15,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu ongezeko la wagonjwa wa Surua nchini. |
Na Okuly Julius-Dodoma
Kwa tathmini iliyofanyika kwa kuchambua takwimu za miaka mitatu mfululizo yaani mwaka 2019, 2020 na 2021, imeonesha kuwa kiwango cha utoaji wa chanjo za watoto nchini kimeshuka na kinaendelea kushuka.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 15,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu ongezeko la Surua hapa nchini Mhe.Ummy amesema kuwa kuwa baada ya kuwepo ongezeko la wagonjwa wa Surua nchini,Wizara imefanya tathmini ya mwenendo wa utoaji wa chanjo za watoto nchini ili kubaini idadi ya watoto wanaopata na kukamilisha chanjo kwa kuzingatia ratiba.
"Hali hii ya uwepo wa idadi kubwa ya watoto ambao hawajapata chanjo au hawajakamilisha chanjo ikiwemo Chanjo ya Surua inaiweka nchi yetu katika hatari ya kupata milipuko ya magonjwa hususani yaleyanayozuilka kwa chanjo,"Amesema Ummy
Na kuongeza kuwa "Chanjo ya Surua/Rubella hutolewa kwa mtoto anapofikia umri wa miezi 9 kwa dozi ya kwanza na miezi 18 kwa dozi ya pili ili kupata kinga kamili narudia tena kutoa rai kwa umma kupeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wapatiwe chanjo ya Surua/Rubella," Ameongeza
Ummy ametaja Mikoa yenye Watoto wengi ambao hawajapata chanjo (zero dose) ni Kigoma, Kagera, Mara, Songwe,Manyara na Mbeya.
Huku Mikoa yenye Watoto ambao hawaja kamilisha chanjo niTabora, Dar es Salaam, Arusha, Geita, Rukwa, Shinyanga, Manyara, Pwani,Singida, Ruvuma, Dodoma, Kigoma, Morogoro, Lindi, Songwe, Mtwara,Katavi, Iringa na Mbeya.
Ummy amebainisha moja ya sababu zinazotajwa kuathri utoaji wa chanjo ni janga la UVIKO 19. Sababu hii haijaathiri tu Tanzania bali nchi nyingi duniani.
Jumla ya wagonjwa wote waliothibitika kuwa na maambukizi ya Surua imefikia hamsini na nne (54) kwa kipindi cha Julai hadi Agosti 2022 nchini.
Hata hivyo hakuna kifo kilichotolewa taarifa kutokana na ugonjwa huo ambapo kati ya wagonjwa 54 waliothibitika kuwa na Surua, wagonjwa 48 walikuwa na umri usiozidi miaka 15 na wagonjwa 6 walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 15.
No comments:
Post a Comment