WADAU WA MAENDELEO WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTOA HUDUMA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 4, 2022

WADAU WA MAENDELEO WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTOA HUDUMA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akizungumza leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa elimu Jumuishi Tanzania wa mwaka mmoja 2021/22 ikiwa ni sehemu ya mpango wa miaka mitano 2021/22 - 2025/2026 baada ya mwaka mmoja wa utekelezaji.
Mkurugenzi wa Elimu Maalum, Dk Magreth Matonya Francis Michael akizungumza leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa elimu Jumuishi Tanzania wa mwaka mmoja 2021/22 ikiwa ni sehemu ya mpango wa miaka mitano 2021/22 - 2025/2026.baada ya mwaka mmoja wa utekelezaji
Sehemu ya Washiriki wa kikao kazi cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa elimu Jumuishi Tanzania wa mwaka mmoja 2021/22 ikiwa ni sehemu ya mpango wa miaka mitano 2021/22 - 2025/2026.baada ya mwaka mmoja wa utekelezajiSehemu

Na Okuly Julius-Dodoma

SERIKALI imewataka wadau wa maendeleo waendelee kuona umuhimu wa kuchangia juhudi za serikali katika kuwapatia huduma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ujifunzaji na kutimiza ndoto zao.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 4,2022 Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael wakati akifungua kikao kazi cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa elimu Jumuishi Tanzania wa mwaka mmoja 2021/22 ikiwa ni sehemu ya mpango wa miaka mitano 2021/22 - 2025/2026.baada ya mwaka mmoja wa utekelezaji


Dk Michael amesema kipaumbele kiwekwe katika uboreshaji wa mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji hususani kwenye shule, vyuo vya ualimu, vyuo vya maendeleo ya wananchi, vyuo vya ufundi stadi na vikuu.

“Natoa wito kwa viongozi wa taasisi zinazojihusisha na utoaji elimu jumuishi, ziendelee kushirikiana na serikali kuhamasisha umuhimu wa elimu kwa watu wenye mahitaji maalum,”alisema.

Aidha, amewaomba wadau wa elimu jumuishi kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa wote unazingatia ujumuishi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa na jitihada anazoonesha kwa watu wenye ulemavu kwa kukutana nao kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazowakabili katika maisha yao...

Mwaka huu amepata nafasi ya kukutana na wanafunzi viziwi wanaosoma katika shule ya sekondari Benjamin na kuongea nao kwa upendo,”amesema .

Na kuongeza kuwa:”Pia aliandaa hafla ya kuongea na kula chakula cha pamoja na watu wenye ulemavu wa Tanzania Bara na Zanzibar hii inaonesha jinsi anavyowajali, anavyowathamini na anavyowakubali,”.

Dk Michael amesema lengo la kikao hicho ni kupata uelewa kuhusu mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26, kufanya mawasilisho ya serikali na wadau kuhusu utekelezaji wa mkakati huo na kufanya tathimini kwa mwaka wa kwanza.

Aidha, kugawa kazi za kufanya mwaka wa pili wa mkakati 2022/23 kwa kuangalia mikoa na wilaya ambazo hazina wadau wa Elimu Jumuishi ikiwemo mikoa ya Kigoma, Songwe, Katavi na Rukwa.

Pia, kufanya majadiliano kuhusu miongozo ya ziara ya nyumbani, shule ya nyumbani na uanishwaji na usimamizi wa shule maalum na jumuishi na kutoa maoni ya kuboresha sera, mitaala kuhusu elimu hiyo ngazi zote za elimu.

“Kikao hiki ni muhimu kwani kinajadili namna ya kuboresha utoaji elimu Jumuishi nchini kwa kufanya tathimini ya utekelezaji na kubaini changamoto mbalimbali na kutafuta muafaka ili kutoa huduma bora kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum,”amesisitiza Dkt.Michael

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Elimu Maalum, Dk Magreth Matonya alisema kupitia kikao hicho kutakuwa na upokeaji maoni kuhusu namna ya kuboresha sera na mitaala ya elimu ili kundi hilo lihusishwe ndani yake.

No comments:

Post a Comment