![]() |
Mkurugenzi wa SOS David Mulongo akitoa Maelezo muda mfupi kabla yakukabidhi Komputa kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum. |
![]() |
Baadhinya Watumishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum waliohudhuria yaugawaji wa Vitendea kazi Komputa viluvyotolewa na Mdau SOS kwa Wizara hiyo. |
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM)
Na MJJWM, DODOMA
Shirika la Children's SOS Village limeikabidhi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum Kompyuta sita zenya thamani ya zaidi ya Mil. 14 aina HP Brobook shabaha ikiwa ni kuboresha utendajikazi wa kila siku kwa wataalam wa Wizara hiyo.
Hafla ya Mapokezi hayo imefanyika leo Oktoba, 07, 2022 na Kuongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Patrick Golwike, katika Ofisi za Wizara zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo Menejimenti na wataalam kutoka Wizara hiyo, wameshuhudia mapokezi hayo huku wakilipongezaa shirika hilo kwa mchango wake wanaoendelea kuutoa kwa Serikali.
Akipokea Komputa hizo, Kaimu Katibu Mkuu Golwike amewashukuru SOS kwa msaada huo na misaada mingine ambayo shirika hilo imekuwa ikiitoa katika maeneo mbali mbali nchini kwa ajili yakuboresha huduma kwa jamii ya watanzania.
“Mlichokileta hapa leo sio kidogo, ni kikubwa sana kwani upatikanaji wa koputa hizo utachochoea na kumfanya mfanyakazi kufanya kazi zake muda wote na mahali popote akiwa na Komputa kwania kweli bado tunauhitaji kutokaana na mabadiliko ya Teknoljia na vifaa vyetu vingi ukiviangalia unakuta zimepitwa na wakati” amesema Gwolwike.
Golwilke amewataka watumishi watakaopata sehemu ya Kompyuta hizo, kuzitunza na kufanyia kazi kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwepo kuboresha kazi zao.
Akitoa Salaam za Shirika, Mkurugenzi wa Shirika hilo David Mulongo, amesema Dunia ikiwa inahama na kuachana na matumizi ya Makaratasi wameona ni muda muafaka wa kurahisisha utendaji kwakuunga Mkono jitihada mbali mbali zinazofanywa kwakutoa vitendea kazi kwa Wizara ili watumishi wake waweze kutekeleza majukumu yao.
“Dunia ikiwa inahama kutoka kwenye paper work na kuhamia kwenye paperless ni wakati muafaka pia kuboresha utedaji wa kazi, tulipokea maombi yakufanya uwezeshaji wa vitendea kazi nasi ka SOS tukaona ni wakati muafanka “ amesema Mulongo
Awali akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu, kuzungumza Naibu Kamishna wa ustawi wa Jamii, Baraka Makona alisema SOS Children’s wameendelea kuwa wa mfano katika kushirikiana na Serikali, na kutoa michango yao ya hali na mali ili kuwawezesha wataalam wa Serikali.
Katika hatua nyingine Bwana David Mulongo amewaambia wajumbe walihudhuria hafla hiyo kuwa kwa sasa wamekamilisha andiko litakalo Kwenda kutatua changamoto za watoto waishio kwenye Mazingira ya Mtaani na kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment