Klabu ya Yanga SC imepangwa kucheza na Club Africain kutoka Tunisia kwenye michezo ya mtoano kutafuta timu zitakazoingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mechi ya kwanza ya mtoano kupigwa Novemba 02, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na marudiano kuchezwa Novemba 09, 2022.
Club Africain ndio walioifunga timu ya Kipanga ya Zanzibar bao 7-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani Stade Olympique Hammadi Agrebi huko Radès, Tunis, Tunisia. |
No comments:
Post a Comment